Ni mpenzi wa lugha ya Kiswahili. Licha ya kuwa ni mhariri na mwandishi wa vitabu, mimi pia ni mfasiri. Nafasiri maandiko kutoka lugha ya Kiingereza kuja Kiswahili na kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Pia ni mwanablogu: http://simbadeo.wordpress.com Ndiyo kusema kuwa ninapenda kuperuzi kwenye kurasa za mtandaoni ili kuilisha akili kwa habari mbalimbali zinazojiri huku na huko duniani. Ni raia wa Tanzania na mkaazi wa Dar es Salaam. Karibu.
makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mosi Simba kutoka Agosti, 2012
Nigeria: Rais wa Seneti Atakiwa Kuwataja Wafadhili wa Boko Haram
Makundi mawili ya vijana Kaskazini mwa Nigeria Jumatano yalimkosoa Rais wa Seneti, David Mark, kutokana na matamshi aliyotoa siku za karibuni akiwataka viongozi wa mikoa ya kaskazini kudhibiti shughuli za kundi linaloogopwa sana la Boko Haram, Connected Africa anaripoti.
Brazil: Mtoto wa Miaka 13 Aonyesha Matatizo ya Shule Kupitia Facebook
Diário de Classe [pt], ukurasa wa Facebook uliofunguliwa na Isadora Faber, aliye na miaka 13 na anayetokea Santa Catarina, Brazil, tayari umeonyesha kupendwa zaidi ya mara 176,000. Huku lengo lake likiwa ni “kuonyesha ukweli kuhusu shule za umma”, Isadora anaweka picha zinazoonyesha maeneo yanayohitaji kufanyiwa ukarabati katika shule yake pamoja na...
Kocha wa Timu ya Taifa ya Zambia Atunukiwa Ukaazi wa Kudumu
Zambia imewahi kuwa na makocha wengi wa kigeni wa timu ya Taifa ya soka, lakini ni Mfaransa Herve Renard, aliyeongoza timu hiyo hadi kushina Kombe la Washindi Barani Afrika mwaka 2012, aliyepata upendeleo wa pekee. Ili kutambua mafanikio yake haya, serikali imemtunuku ukaazi wa kudumu lakini uamuzi huo unaonekana kuwekewa chumvi ya kisiasa.
Serikali ya Kolumbia Yapanga Kufanya Mazungumzo na Waasi wa FARC
Katika blogu ya Crónicas, Santos García Zapata anaeleza muktadha [es] kuhusu uamuzi wa Rais wa kuanzisha mazungumzo ya amani na makundi ya waasi. Kongresi ya ‘Kamisheni ya Amani’ imetangaza kwamba Rais Santos “hayupo peke yake” katika dhamira yake ya kupatikana kwa amani.
Sudani: Mwanaharakati Mtumia Twita Aachiwa Huru
'Nilitishiwa kufanyiwa vitendo vya ngono na kutendewa vibaya mara kadhaa katika siku ile. Wakati mmoja hata na ofisa wa ngazi za juu wa #NISS.' Mwezi Juni, Shirika la Ujasusi na Usalama wa Taifa la Sudani liliwakamata maelfu ikiwa ni pamoja na mwanaharakati anayetumia Twita Usamah Mohamed Ali.
Iran: ‘Marufuku Isiyo Rasmi ya Kutembea’ ya Tehran Wakati wa Mkutano wa NAM
Mkutano wa 16 wa Umoja wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote ulianza mnamo tarehe 26 Agosti, 2012 jijini Tehran huku kukiwa na ulinzi mkali. Umoja huo madhubuti (NAM) unaoundwa na nchi ni mabaki ya mvutano uliokuwepo enzi za Vita Baridi kati ya Mashariki na Magharibi, na umoja huu unachukuliwa na Iran pamoja na mataifa mengine kama jukwaa mbadala kwa ajili ya kuendesha mijadala kuhusu masuala mbalimbali yanaoukabili ulimwengu hivi sasa. Iran inasema inapanga mazungumzo kuhusu mpango wa amani ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, lakini hakuna uwakilishi kutoka upande wa waasi ulioalikwa kwa sababu Tehran ni rafiki wa karibu wa utawala wa Rais Bashar Assad wa Syria.
Mgogoro wa Umoja wa Ulaya: Kitabu cha Kwanza cha Global Voices cha Kieletroni
"Umoja wa Ulaya katika Mgogoro" (EU in Crisis) ni chapisho letu la kwanza katika Mradi wa Vitabu wa Global Voices na ambao unahusisha makala bora zaidi kuhusu mazungumzo ya kijamii, ushiriki na uhamasishaji unaopewa nguvu na raia wanaopitia nyakati ngumu za kubana matumizi katika bara la kale zaidi na kwingineko.
Tanzania, Ethiopia: Meles Zenawi ‘Atuma Twiti’ Kutoka Kilindi cha Kaburi
"@zittokabwe tafadhali uwe bora kuliko mimi nilivyokuwa. Huku juu hakuna utani, tayari ninalipia makosa yangu." Twiti iliyotumwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi baada ya kifo chake kwenda kwa Mbunge wa Tanzania Zitto Kabwe na kuibua mjadala mtandaoni.