Mosi Simba · Machi, 2010

Ni mpenzi wa lugha ya Kiswahili. Licha ya kuwa ni mhariri na mwandishi wa vitabu, mimi pia ni mfasiri. Nafasiri maandiko kutoka lugha ya Kiingereza kuja Kiswahili na kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Pia ni mwanablogu: http://simbadeo.wordpress.com Ndiyo kusema kuwa ninapenda kuperuzi kwenye kurasa za mtandaoni ili kuilisha akili kwa habari mbalimbali zinazojiri huku na huko duniani. Ni raia wa Tanzania na mkaazi wa Dar es Salaam. Karibu.

Anwani ya Barua Pepe Mosi Simba

makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mosi Simba kutoka Machi, 2010

Serikali ya Japani: Kuhusu Kuanguka kwa Mfumo wa Ajira

  31 Machi 2010

Chombo kinachotumika kufanya tafakari nzito cha Baraza la Mawaziri la Japani, Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (内閣府 経済社会総合研究所)(ESRI) kimechapisha matokeo ya utafiti yaliyopima hadhi ya sasa ya ajira ya maisha na ulipaji ujira kwa kutumia cheo cha mtu (yaani, mfumo wa ajira wa Kijapani). Walitumia data (1989 –...

China: Uchi Ulio Rasmi

  26 Machi 2010

Serikali moja ya mji huko katika Jimbo la Sichuan sasa inaitwa “Serikali ya Kwanza nchini China Iliyo Uchi kabisa” baada ya kuwa maafisa wa mji huo kuweka mishahara na matumizi ya serikali kwenye tovuti. Kutajwa kwa suala la ‘uchi au utupu’ katika machapisho mengi ya Kichina katika siku za karibuni...

Misri: Wafanyakazi wa IslamOnline Wagoma

Mamia ya wafanyakazi, wahariri, na waandishi wa habari walianza mgomo wa kuonyesha hasira yao katika mtandao unaosomwa sana wa jiji la Cairo unaojulikana kwa jina la Islamonline baada ya kuwa wafanyakazi wapatao 250 wamefukuzwa kazi. Kwa mara ya kwanza, wagomaji wanatumia kwa ufanisi na vizuri kabisa aina mpya ya chombo cha habari ili kuvuta usikivu na uungwaji mkono katika kile wanachokipigania, kuanzia na Twita inayoendelea mpaka mmiminiko wa habari wa hapo kwa hapo.