Ni mpenzi wa lugha ya Kiswahili. Licha ya kuwa ni mhariri na mwandishi wa vitabu, mimi pia ni mfasiri. Nafasiri maandiko kutoka lugha ya Kiingereza kuja Kiswahili na kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Pia ni mwanablogu: http://simbadeo.wordpress.com Ndiyo kusema kuwa ninapenda kuperuzi kwenye kurasa za mtandaoni ili kuilisha akili kwa habari mbalimbali zinazojiri huku na huko duniani. Ni raia wa Tanzania na mkaazi wa Dar es Salaam. Karibu.
makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mosi Simba kutoka Agosti, 2008
Waziri matatani kwa cheti ‘feki’
Ali Kordan,Waziri wa Mambo ya Ndani wa Irani, Katika siku za hivi karibuni, ameshutumiwa vikali kwa kuonyesha Shahada ‘feki’ ya Udaktari (PhD) aliyodai kupata kutoka katika chuo kikuu chenye sifa kubwa duniani cha Oxford cha nchini Uingereza. Tovuti mbalimbali, pamoja na ile ya kihafidhina wa Alef, zimechapisha picha ya cheti...
Pakistani: Musharraf Aondoka Jengoni
Imepita miaka nane, siku mia tatu na ushee tangu mapinduzi yasiyo ya kumwaga damu yaliyoongozwa na Jenerali wa Jeshi la Pakistani yalipofanyika na hivyo kumpokonya madaraka kiongozi fisadi Nawaz Sharif. Wakati huo kulikuwa na matumaini ya kesho mpya, ilikuwa ni mwendo wa madaha kuelekea kwenye dira iliyofifia iliyopachikwa jina la...
Korea: Wajibu wa Kitaifa Wachuana na Dhamiri
Kijana mmoja anayetumikia jeshi kama askari polisi aliamua kutorudi kwenye kikosi alichokuwa akifanya kazi baada ya likizo na alipeleka taarifa kuwa dhamiri yake ilikuwa ikimshtaki. Sababu ilikuwa kwamba dhamiri yake ilimshtaki baada ya kuwa amewanyanyasa raia walioshiriki katika mkesha wa tukio la kuwasha mishumaa. Uamuzi wa kijana huyu umevuta hisia...