makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mosi Simba kutoka Julai, 2010
Thailand: Vurugu Zinazotokana na Ujumbe Mfupi wa Maneno wa Waziri Mkuu
Wakati Waziri mkuu wa Thailand Abhisit Vejjajiva alipotwaa madaraka mwaka 2008, alituma ujumbe mfupi wa maneno kwa mamilioni ya wateja wa simu za viganjani wa Thailand akiwataka wawe na umoja. Hivi sasa anakabiliwa na makosa ya ufisadi kwa kupokea "zawadi" kutoka mashirika ya mawasiliano. Kadhalika anashutumiwa kwa kuvunja mipaka ya ya faragha za wateja wa simu za viganjani.
Palestina: Mateso ya Kuwa Uhamishoni
Wakimbizi wa Kipalestina ni miongoni mwa watu ambao wamejikuta wakikimbilia uhamishoni ulimwenguni kote, Umoja wa Mataifa unatoa msaada kwa jumla ya wakimbizi waliosajiliwa wapatao milioni 4.7 katika ukanda unaokaliwa kwa nguvu huko Palestina, Jordan, Lebanoni na Syria. Mamilioni ya wakimbizi wa Kipalestina na wale walioteguliwa kutoka kwenye makazi yao wanaishi sehemu mbalimbali duniani. However, their Hata hivyo, watu hawa daima mioyo yao ipo nyumbani kwao, au kwa wazazi au mababu na mabibi zao waliobaki nyuma. Wanablogu wawili wa huko Gaza wameandika kuhusu mateso ya kuwa uhamishoni.
Ivory Coast: Mwanablogu na Mwandishi wa Habari Théophile Kouamouo Akamatwa Pamoja na Timu Yake Tangu Julai 13
Waandishi wa habari watatu wa Le Nouveau Courrier d'Abidjan walitiwa mbaroni na polisi baada ya kukataa kueleza vyanzo vya habari vya uandishi wao wa kipelelezi kuhusu biashara ya usafirishaji kahawa na kakao kwenda nje ya nchi. Yafuatayo ni maoni kutoka kwa raia na vyombo vya habari nchini Ivory Coast huku wenzao watatu wakiendelea kupigania kuachiwa kwa wanahabari hao.
Rwanda: Wanaomuunga Mkono wa Paul Kagame Wabaini Nguvu ya Twitter, Facebook na Blogu
Waungaji mkono wa rais Paul Kagame wa Rwanda wameanza kutumia nguvu ya ushawishi ya Facebook, Twitter na blogu ili kumsaidia kushinda uchaguzi wa rais unaotarajiwa kufanyika tarehe 9 Agosti 2010.
Afrika ya Kusini: Dakika 67 za Mabadikio – Siku ya Mandela
Nelson Mandela alitumikia kifungo cha miaka 27 jela kule katika Kisiwa cha Robben, Afrika Kusini. Kitu ambacho watu wengi hawajui ni kwamba Madiba (kama ambavyo wengi wanapenda kumwita huko Afrika ya Kusini) alitumia miaka 67 ya maisha yake katika kupiga vita ubaguzi wa rangi na umaskini. Jumapili hii Julai 18 2010, kutakuwa na maadhimisho ya miaka yake 92 - na pia Siku ya Mandela - siku ambayo watu duniani kote watajitolea dakika 67 ili kuifanya dunia iwe sehemu nzuri ya kuishi kwa wote.
China: Kashfa ya Wizi wa Kitaaluma Uliofanywa na Wang Hui, Mtazamo wa Kimataifa
Kuna kashfa ya wizi wa kitaaluma iliyoibuka mwezi Machi katika duru za kitaaluma za Kichina pale Profesa wa Fasihi wa Chuo Kikuu cha Nanjing, Wang Binbin, alipotuhumu kwamba kazi ya...
Uganda: Wanablogu Washtushwa na Milipuko ya Mabomu
Mashabiki wa soka kote ulimwenguni walikusanyika kwenye kumbi za baa na migahawa ili kushuhudia mechi ya fainali za Kombe la Dunia usiku wa Jumapili iliyopita. Nchini uganda usherehekeaji huu ulikatishwa pale milipuko ya mabomu iliposambaratisha maeneo mawili maarufu kwa sherehe za mpaka majogoo jijini Kampala, mji mkuu wa nchi hiyo.
Naijeria: Nani Amemfanya Rais Abadili Msimamo — Facebook au FIFA?
Baada ya kupokea mamia ya maoni kwenye ukurasa wake wa Facebook page, Rais wa Naijeria alibadili uamuzi wake tata wa kuifungia timu ya taifa ya nchi hiyo. Lakini je ni kweli kwamba kubadilika huku kwa moyo wa Jonathan kulitokana na maoni ya raia waliopaaza sauti zao zenye hasira katika Facebook? Au ulitokana na msukumo wa shirikisho lenye nguvu la mpira wa miguu?
Kambodia: Je, Viwango vya Maadili Miongoni Mwa Watawa Vinaporomoka?
Mtawa nchini Kambodia alikamatwa kwa akichukua picha za video za wanawake waliokuwa uchi katika jumba la watawa. picha hizo za video zilisambazwa sana kwa kutumia simu za viganjani na intaneti. Pia kuna taarifa nyingine za watawa kulewa na kuangalia filamu za ngono. Wanamtandao wa Kambodia wanatoa maoni