makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mosi Simba kutoka Oktoba, 2009
Caribbean: Tafakari Mpya Kuhusu Uchapishaji wa Mtandaoni
Wanablogu wa ukanda wa Karibea wanawaza kuanzisha jumuiya ya uandishi na uchapishaji ya mtandaoni ikitumia njia za mawasiliano zilizo shirikishi ili kukabiliana na ugumu wa uchapishaji vitabu unaoukabili ukanda wao.
Uanaharakati na Umama Barani Asia
Je, mwanamke anatoa sadaka zipi ili kupigania jambo analiamini? Je, watoto wake wanaathiriwa vipi na mateso yanayoelekezwa kwake? Makala hii inachambua kwa kifupi maisha ya wanawake wanaharakati katika Asia ambao pia ni ma-mama.
China: Ndoto ya Nobel
Kila mwaka, wakati wa kutangaza mshindi wa Tuzo ya Nobel unapowadia, Wachina hugubikwa na hamasa fulani hivi. Endapo mshindi ni yule wa asili ya Uchina, basi wao hufurahi sana. Lakini mara baada ya kupita siku chache, furaha hiyo huanza kupoa au hata kugeuka na kuwa simanzi. Mwaka unaofuata wakati unapowadia tena, hali hujirudia tena kama hapo awali.