makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mosi Simba kutoka Septemba, 2008
Sheria inapokwaza haki za binadamu …
Mtoto mwenye umri wa shule ya msingi aliyepatikana nje ya ndoa huko Zhuhai, kusini mwa China, hakubaliwi kujiunga na shule, kwa sababu mama yake hawezi kulipa faini kubwa ya kuwa na "mwana haramu", habari hii inasimuliwa na bloga, Han Tao.
Colombia: Watu Wanaswa na Mitego ya Upatu
Kwa kupitia picha za video na mtandao wa marafiki wa Facebook, raia wa Colombia, Diego Alejandro, anaweka wazi udanganyifu na utapeli mkubwa uliojificha nyuma ya michezo ya upatu ambayo inatangazwa kama njia mbadala za uwekezaji. Katika nchi ambapo akaunti za benki zimepoteza maana kwa sababu ada za uendeshaji ziko juu kuliko riba anayopata mwenye akaunti, michezo hii ya upatu inayoshawishi kumjaza mtu mapesa, ambapo raia wanalipa kiasi fulani cha pesa ili kujiunga na kisha kuingiza marafiki zao 7 kabla wao hawajaanza kufurahia riba ya juu ajabu (kati ya asilimia 40 mpaka 70) basi imekuwa ni kivutio kikubwa mno.
Venezuela: Wahindi wa Yukpa, Chavez na Mgogoro wa Ardhi
Picha za video zinazotumwa kwenye mtandao wa internet na vyombo vya habari vya kiraia zinaonyesha yale yanayojiri kuhusu mgogoro unaoibuka nchini Venezuela kati ya Wahindi wa jamii ya Yukpa wanaoishi katika milima ya Perijá, wamiliki wa ardhi na Rais Chávez. Mgogoro huu kuhusu mipaka ya ardhi umekuwapo kwa takribani miaka 30, yaani tangu pale vikosi vya jeshi vilipowandoa kwa nguvu wanajamii wenyeji ya Ki-Yukpa na kuwapa ardhi hiyo wamiliki wapya walioanzisha mashamba makubwa ya mifugo, hasa ng'ombe, ambao wameendelea kuitumia ardhi hiyo tangu wakati huo.