Ni mpenzi wa lugha ya Kiswahili. Licha ya kuwa ni mhariri na mwandishi wa vitabu, mimi pia ni mfasiri. Nafasiri maandiko kutoka lugha ya Kiingereza kuja Kiswahili na kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Pia ni mwanablogu: http://simbadeo.wordpress.com Ndiyo kusema kuwa ninapenda kuperuzi kwenye kurasa za mtandaoni ili kuilisha akili kwa habari mbalimbali zinazojiri huku na huko duniani. Ni raia wa Tanzania na mkaazi wa Dar es Salaam. Karibu.
makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mosi Simba kutoka Aprili, 2011
Misri: Mubarak awekwa Kizuizini
Miezi michache tu iliyopita, raia wengi wa Misri walitamani sana kumwona aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Rais Mubarak, akitupwa jela, hata hivyo, pengine ni wachache miongoni mwao waliofikiri kwa uhakika kabisa kwamba siku moja jambo hili lingetimia. Hata hivyo, mnamo Jumatano ya tarehe 13 Aprili, 2011, raia wa Misri waliamka na mapema asubuhi ya siku hiyohiyo kukutana na habari zinazohusu Mubaraka kutupwa kizuizini. Hapa chini tunawaletea jinsi habari hizi zilivyopokelewa katika ulimwengu wa uandishi wa habari wa Kijmii miongoni mwa Wamisri.
Ivory Coast: Je, nani anadhibiti televisheni ya taifa ya RTI?
Bado kuna mkanganyiko kuhusu swali la nani hivi sasa ndiye mwenye udhibiti wa Radio Télévision Ivoirienne (RTI) , ambacho ni kituo cha televisheni ya taifa.
Myanmar: Simulizi za Wafanyakazi wa Misaada Baada ya Tetemeko la Ardhi
Myanmar bado inasumbuka kutokana na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.8 ambalo liliikumba nchi hiyo. Mwandishi wetu aliyeko Myanmar anatafsiri mahojiano na simulizi za wakazi pamoja na wafanyakazi wa misaada ambao walishuhudia kiwango cha uharibifu uliofanywa na tetemeko hilo kaskazini mashariki mwa Myanmar.
Bahrain: Waandishi wa Habari Wazuiwa Kuingia Wakiwa Uwanja wa Ndege
Bahrain iliingia kwenye vurugu kubwa zilizoambatana na polisi kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji waliopiga kambi katika eneo muhimu la wazi linalohusudiwa sana liitwalo Lulu Jumatano iliyopita. Mchana wa siku hiyo nilipanda ndege inayotoka Doha, nchini Qatar, kwenda Bahrain, kwa upande mmoja nikitaka kujionea mwenyewe nini kilikuwa kikitokea katika nchi hii ya kisiwa ambayo ilipata kuwa nyumbani kwangu. Saa kadhaa baadaye nilijikuta kwenye ndege ya kurudi Doha, baada ya kunyimwa ruhusa ya kupita pale uwanja wa ndege.
Wanablogu wa Kenya Waunda Umoja; BAKE
Mnamo tarehe 25 Machi, wanablogu kadhaa wa Kenya walifanya mkutano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi, mkutano uliitishwa na BAKE (Bloggers Association KEnya). Huo ulikuwa mkutano wa 4 uliotokana na msukumo wa wanablogu wakongwe wa Kenya.
Saudi Arabia: Mfalme Awaahidi Wananchi wa Saudia Fedha Zaidi
Fedha zaidi zimeahidiwa kutolewa kwa wananchi wa Saudia, ahadi ambayo Mfalme Abdulla ameitoa kupitia hotuba yake kwa taifa leo. Katika hotuba hiyo iliyokuwa fupi, Mlinzi wa Misikiti Miwili Mitukufu aliwashukuru viongozi wa dini, waandishi na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa juhudi walizofanya kutetea ufalme. Matamko na Amri vilifuata ya kwamba mabilioni yatagawanywa kwa watu wa Saudia.