Fedha zaidi zimeahidiwa kutolewa kwa wananchi wa Saudia, ahadi ambayo Mfalme Abdulla ameitoa kupitia hotuba yake kwa taifa leo. Katika hotuba hiyo iliyokuwa fupi, Mlinzi wa Misikiti Miwili Mitukufu aliwashukuru viongozi wa dini, waandishi na Wizara ya Mambo ya Ndani kwa juhudi walizofanya kutetea ufalme. Baada ya hapo, matamko kadhaa yalisomwa na mtangazaji, hasa akieleza jinsi mabilioni ya dola yatakavyotumika katika kujenga nyumba bora, kazi na afya kwa raia wote wa Saudia. Vilevile kuna mpango wa kuunda kamati ya kudhibiti rushwa; wafanyakazi wa Saudia watanufaika na kima cha chini cha mshahara; wakati ambapo wanajeshi na askari polisi watapandishwa vyeo kama wanavyostahili.
Hotuba hii imevuta hisia za raia wa mtandaoni, kabla, wakati na baada ya kusomwa kwake. Katika Twita alama #sakingspeech ilikuwa mada inayoenea kwa kasi ulimwenguni kote.
Hotuba hiyo ilikuja baada ya miito, maandamano madogo kudai mageuzi katika falme hiyo, ambapo viongozi wa dini hapo wali waliwaasa WaSaudia kutodandia wimbi la maandamano ya upinzani linaloikumba kanda hiyo kwani maandamanio ya namna hiyo ndani ya Saudi Arabia ni kinyume na dini. Kwa nasibu, moja ya amri za kifalme zilizotolewa leo ilikuwa ni kuundwa kwa chombo kipya cha kidinikitachoshughulikia fatwa (amri za kidini).
Hapa kuna baadhi ya yale yaliyosemwa katika Twita kufuatia hotuba na amri za mfalme wa Saudia:
@khalidalkhalifa: Mtukufu Mfalme Abdalla wa Saudi Arabia atazungumza hivi punde kwenye Televisheni … ulimwengu tegeni masikio yenu.
@sultanalqassemi: Mfalme wa Saudi Arabia awashukuru viongozi wa dini, waandishi & Wizara ya Mambo ya Ndani kwa juhudi zao za kuulinda ufalme.
@SultanAlQassemi: Ufalme wawashukuru & kuwasifu viongozi wa dini ya Kiislamu kwa zaidi ya dakika moja #Saudi
@afaliq:Ikiwa ningetakiwa kutoa muhtasari wa hotuba ya mfalme katika maneno matano ningesema “asanteni – haya fedha zaidi hizi hapa” #SAkingspeech
@jenanmoussa: mfalme wa #Saudi azungumzia taratibu mpya. Kiasi cha riyali 2000 zitatolewa kila mwezi kwa kila mmoja asiye na ajira. #KSA
@docshayji: Mfalme Abdudllah wa #KSA ametoa matamko ambayo baadhi yake ni: motisha wa mshahara wa miezi miwili kwa wafanyakazi wote raia wa Saudi Arabia & wanafunzi. Riyali 2000 kwa wote wasio na ajira.
@Matthias_Sailer: Mfalme wa #Saudi aamuru mfululizo wa manufaa ya kifedha kwa raia wake: malipo ya motisha, nyongeza ya mshahara wa kima cha chini, mshahara n.k. kupitia SultanAlQassemi #KSA #Gulf
@Saudiwoman: Bilioni 16 kwenda wizara ya afya ili kujenga kituo cha saratani na vitengo vingine muhimu, zahanati na nyumba kwa ajili ya hospitali zote kubwa
@schaefdogschaef: MFALME WA SAUDIA AAMURU KUJENGA NYUMBA ZIPATAZO 500,000 … hiyo bado ni bei nafuu ya kumwezesha kuendelea kubaki madarakani!!
@AnasAlaoui: “Amri ya 7 ya Mfalme wa Saudi Arabia – kuanzisha taasisi ya kudhibiti rushwa itakayosimamiwa moja kwa moja na mfalme, hakuna ambaye hatachunguzwa na taasisi hiyo”
@bagadood: Tamko la 8 la Kifalme: Kuongeza msaada zaidi kwa hospitali binafsi kwa kiasi cha Riyali milioni 200 #SAKingSpeech #SaudiMataleb
@Redbelt: Kwa maoni yangu, tamko kuhusu kiwango cha chini cha mshahara kwa raia wa Saudia ni kibaya sana kwa kutazama mbele zaidi. #ksa
@bagadood: 1Tamko la 10 la Kifalme: Hatua ya kuwapandisha vyeo askari jeshi & polisi wote wanaostahili kufanyiwa hivyo #SAKingSpeech #SaudiMataleb
@alnitak250: #Saudi Mfalme anamwaga fedha/manufaa ya kiuchumi lakini mpaka sasa hakuna dalili za mabadiliko ya kweli ya kidemokrasi
@mahmoodali1: #Saudi Mfalme angeweza kabisa kutuma kwa TWITA hotuba yake kwa herufi zisizozidi 140!#lol #ksa #Bahrain #GCC
@beleidy: Ala, Mfalme wa Saudia amezungumza kwa dakika chache, na amemwaga pesa na fursa za kazi zaidi
@alhefzi: #SAKingSpeech, jamani MAPESA HAYA YOTE yalikuwa wapi!?!?!?! =) =)
@SBassam: Hadi sasa, hakuna maagizo yoyote ya maana kutoka kwa mfalme. Hata hivyo, bado nina matumaini!! #Saudi
@Nuha_Nofal: He! Tutaishiwa fedha jamani, mweee! #SAKingSpeech
@YazzNafjan: #SAKingSpeech ni mada motomoto, hii ni mara ya pili Mfalme wa Saudia anakuwa katika hali hii. #Awesome
Mtumiaji wa Twita Aziz Shalan anatutumia picha inayoonyesha kuenea kwa mada hiyo: