Ni mpenzi wa lugha ya Kiswahili. Licha ya kuwa ni mhariri na mwandishi wa vitabu, mimi pia ni mfasiri. Nafasiri maandiko kutoka lugha ya Kiingereza kuja Kiswahili na kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Pia ni mwanablogu: http://simbadeo.wordpress.com Ndiyo kusema kuwa ninapenda kuperuzi kwenye kurasa za mtandaoni ili kuilisha akili kwa habari mbalimbali zinazojiri huku na huko duniani. Ni raia wa Tanzania na mkaazi wa Dar es Salaam. Karibu.
makala mpya zaidi zilizoandikwa na Mosi Simba kutoka Februari, 2020
Serikali ya Zimbabwe yaendelea kutumia habari za mtandaoni kama silaha ya kukandamiza haki za raia
Serikali mpya, iliyoongozwa na Emmerson Dambudzo Mnangagwa,iling’amua mara nguvu ya mitandao ya kijamii. Kama waziri wa zamani wa usalama wa nchi, Mnangagwa pia alitambua umuhimu na nafasi ya upotoshaji taarifa katika nyanja za kisiasa za Zimbabwe.
Je, Uganda itazima intaneti kadiri upinzani unavyozidi kuwasha moto kuelekea uchaguzi mkuu wa 2021?
Wakati uchaguzi wa 2021 unapokaribia, kuna uwezekano mkubwa kuwa utawala wa Uganda utaendeleza ukandamizaji wa wapinzani, ikiwa ni pamoja na kufunga mitandao ya kijamii.