uhamishoni ulimwenguni kote, ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Wakala wa Kazi (UNRWA) likitoa msaada kwa jumla ya wakimbizi waliosajiliwa wapatao milioni 4.7 katika ukanda unaokaliwa kwa nguvu huko Palestina, Jordan, Lebanon na Syria. Mamilioni ya wahamiaji wa Kipalestina na wale walioteguliwa kutoka kwenye makazi yao Palestinians wanaishi sehemu mbalimbali duniani. However, their Hata hivyo, watu hawa daima mioyo yao ipo nyumbani kwao, au kwa wazazi au mababu na mabibi zao waliobaki nyuma. Wanablogu wawili wa huko Gaza wameandika kuhusu mateso ya kuwa uhamishoni.
Mapema wiki chache zilizopita, meli yenye misaada iliyodhaminiwa na Libya inayoitwa Al-Amal (“matumaini”) ilijaribu kusafiri kwenda kwenye ukanda wa Gaza (lakini ililazimishwa kubadili uelekeo na kwenda Misri). Kule Gaza, mwanablogu Kalam alikuwa akimwazia mtu ambaye yeye angetamani awe kwenye meli hiyo:
ترتدي وشاح الصلاة وتحمل مسبحة بين يديها وتدعو الله عز وجل – أو ربما تفعل فقط كما ترى والديها يفعلان حينما تضيق بهما السبل- فتناجي الله أن يحقق أملها أو بالأحرى أمل جدتها في رؤيتها واحتضانها وتقبيلها.
هي هلا التي لم تكمل سنتها الأولى في الحياة بعد، ولكنها تحمل بالوراثة كل مشاعر الفلسطيني المغترب، فهي ابنة للاجئ لم من يرى من أرضه شبرا واحدا طوال حياته، ولأم تعيش مشتتة الفؤاد بين الوطن والغربة بين الأهل والزوج بين الأم والبيت بين الأخوة والأبناء، فعقلها وجزء مهم من قلبها هناك وأهلها وبقية قلبها وذكرياتها هنا.
Yeye (binti) huvaa ushungi ulio maalumu kwa ajili ya sala na hushika tasbihi mikononi mwake, na humwomba Mungu – au labda hufanya kile ambacho amekuwa akiwaona wazazi wake wakifanya hasa wakati mambo yanapokuwa magumu – anamwomba Mungu afanye maombi yake yatokee kuwa kweli au kwa usahihi zaidi kuifanya ndoto ya bibi yake kumwona yeye, kukumbatia na kumbusu.
Huyu ni Hala, ambaye bado hajatimiza hata mwaka mmoja wa maisha yake, lakini tayari anabeba hisia za kurithi alizo nazo kila Mpalestina anayeishi uhamishoni. Yeye ni binti wa mkimbizi ambaye hajawahi kutia machoni mwake hata kipande kidogo cha ardhi yake maisha yake yote, na wa mama ambaye huishi huku moyo wake ukiwa umegawanyika kati ya nchi ya asili yake na nchi ya kigeni, kati ya familia yake na ndoa yake, kati ya mama yake na nchi yake ya asili, kati ya ndugu aliozaliwa nao na watoto wake wa kuzaa mwenyewe. Sehemu kubwa ya akili na moyo wake ipo kule, wakati familia yake na sehemu iliyobaki ya moyo wake na kumbukumbu zake viko pale alipo.
Hala
Kalam anaendelea:
هلا ابنة أختى الصغيرة التي تعيش في ليبيا ولا تستطيع القدوم إلى غزة – التي أصبحت قبلة الجميع هذه الأيام- تسبح الله عز وجل وتدعوه أن يسمح لها بالقدوم إلى غزة، فهي لا تتمكن من القدوم بسبب صعوبة الحصول على إقامة لها في ليبيا، الأمر الذي لا يضمن لها العودة إلى هناك حيث والدها النازح – لا يمتلك رقم هوية – وبقية عائلتها، تبحث هلا عمن يقول لها “يا هلا بيكي في وطنك”، تبحث عن من يوصلها لحضن جدتها الحنون، التي تعشق أي صورة لها أو مقطع فيديو تظهر فيه.
هلا تنتظر وكلها أمل، أمل أكبر من السفينة الليبية القادمة إلينا هنا، والتي كم تمنيت أن تكون معهم لأقبلها، حين يصلون سأرى في كل واحد منهم جزء من صورة هلا، وسأسألهم لماذا لم تأتوا بـ هلا معكم؟؟؟!!!
Hala ni mpwa wangu mchanga anayeishi nchini Libya na hawezi kuja Gaza – kitu ambacho kimekuwa ndiyo lengo la karibu kila mmoja wetu siku hizi. Msifu Mungu na mwombe amruhusu binti huyu mdogo kuja Gaza … Anashindwa kuja kwa sababu ya ugumu wa kupata kibali cha ukaazi nchini Libya, na jambo hilo lina maana kwamba hawezi kuwa na uhakika wa kurudi pale ambapo baba yake ambaye naye ni mtu aliyeyakimbia makazi yake – hana namba ya kitambulisho – na ndivyo walivyo wengine wote kwenye familia yake. Hala anamtafuta mtu wa kumwambia, “Karibu kwenye nchi yako”, na anamtafuta mtu wa kumsaidia kupata kukumbatiwa kwa upendo mkubwa na bibi yake, ambaye hupokea kila picha au kipande cha picha ya video inayomwonyesha binti huyu mdogo kwa shauku kubwa kupindukia.
Hala anasuburi matumaini kamili, matumaini yaliyo makubwa kuliko meli ya Libya inayoelekea kuja hapa, ambayo mimi nimetamani sana kwamba yeye angekuwa mmoja kati ya wale walio kwenye meli hiyo ili nami nipate kumkumbatia; watakapofika nitaona ndani ya kila mmoja atakayekuja na hiyo meli kipande kidogo cha picha ya Hala, na nitawauliza kwa nini hawakumchukua Hala pamoja nao.
Vilevile kule Gaza, Kawther Abu Hani anamsikiliza mama yake akielezea kumbukumbu alizonazo:
نفسي اعرف شو صار لبيتنا الصغير اللي تركنا في الناصرة قبل سنين, كيف صار شكل الجبل؟ و يمكن تغيرت ريحة الزعتر؟.. قديش كبرن صحباتي و صرت عندهن مجرد حكاية لاولادهن.. يا الله حتى ما احضرت عرسهن, كان نفسي اعيش مراحل عمري معهن و أكتر شي كنت استنى اليوم اللي نوعى فيه ع الحب و ننسى اللعب تنحب حتى ننهم.. يا الله بس هم الحب مش زي هم الاحتلال. اسا انا اتزكرت.. دايما بتزكر..
“Ningependa kujua nini kiliipata nyumba yetu ndogo tuliyoiacha kule
Nazareti miaka mingi iliyopita … Hivi, vile vilima siku hizi vinaonekana vipi? Na labda ile harufu nzuri ya mimea imebadilika … Hivi, wale rafiki zangu hivi sasa wamekuwa wakubwa kiasi gani, na pengine mimi nimeishia tu kuwa moja ya simulizi kwa watoto wao…Mungu wangu, hata sikupata fursa ya kushiriki kwenye harusi zao. Nilitamani sana kuishi maisha yangu nikiwa miongoni mwao, na zaidi sana nilikuwa nikisubiri ile siku ambapo tungejifunza kuhusu upendo na kusahau kuhusu michezo, kipindi ambacho nasi tungeingia kwenye mapenzi na kujikuta tukihuzunishwa nayo. Mungu wangu, lakini kumbukumbu za upendo si sawa na mashaka ya kuwa chini ya ukandamizaji (wa Waisraeli). Sasa nakumbuka …” Daima yeye hukumbuka hayo.