“Umoja wa Ulaya katika Mgogoro (EU in Crisis)” ni chapisho letu la kwanza katika Mradi wa Vitabu wa Global Voices na ambao unahusisha makala bora zaidi kuhusu mazungumzo ya kijamii, ushiriki na uhamasishaji unaopewa nguvu na raia wanaopitia nyakati ngumu za kubana matumizi katika bara la kale zaidi na kwingineko.
Tulichakua kwa makini kabisa makala zilizokuwa bora zaidi kutoka katika mfululizo wetu wa kuhusu Mgogoro wa Kiuchumi wa Ulaya ambapo mfululizo huo ulianza Majira ya Machipuo ya 2011, na kuandikwa na vikundi vya waandishi wetu wa kimataifa wanaofanya kazi kwa bidii kama waandishi wa kiraia.
Kitabu hicho cha kielektroni kimetolewa kwa utaratibu wa Leseni ya Creative Commons Attribution 3.0 na kinapatikana kwa kukipakua kutoka mtandaoni katika mitindo mitatu tofauti:
- PDF (3,2 MB)
– ePub (3,2 MB)
– Ukubwa wa Mfukoni (2,8 MB)
Kitabu hicho kinapatikana kikiwa na utangulizi halisi kabisa unaofafanua muktadha mpana zaidi kuhusu suala hili. Kitabu hiki cha kieletroniki kina jumla ya makala 13 katika lugha ya Kiingereza (matoleo katika lugha nyingine yanaandaliwa). Makala hizo zimeandikwa kuhusu Ugiriki, Hispania, Ureno, Italia na nchi nyingine za Ulaya, hasa zilizoathiriwa na mgogoro wa kibenki na sarafu ya euro, na mgogoro huo unatazamwa kupitia darubini ya ushiriki wa vyombo vya habari vya kiraia vya mtandaoni.
Kitabu hiki cha kielektroniki kinakusudiwa kuwa zana mojawapo inayoweza kutumiwa kulingana na mazingira na kusambaza zaidi na kuibua mijadala kuhusu masuala haya ya migogoro ya kiuchumi yanayoendelea.
Hadi kufikia mwezi Julai 2012, timu ya watu wetu wanaojitolea wapatao 80 waliandika zaidi ya makala 80 katika lugha ya Kiingereza, makala hizo pia zilitafsiriwa katika lugha nyingi mbalimbali.
Mradi wa Vitabu wa Global Voices unalenga “kushirikisha vyombo vya habari vya kiraia kwa ajili ya siku za baadaye“, kama ambavyo kichwa chetu kidogo kinavyosomeka, kwa kutumia hifadhi kubwa ya GV na uzalishaji wake unaoendelea katika lugha nyingi mbalimbali. Tutakuwa tukitoa matoleo ya vitabu vyetu hivi vya kielektroni kwa kufuata mada, kanda, masuala, lugha, vyombo vya habari n.k. na kwa mitindo mbalimbali, na kwa hiyo kutoa picha pana zaidi na kusambaza zaidi makala zilizo bora zilizoandikwa katika vipindi tofautitofauti kupitia jumuiya yetu.
Tafadhali eneza taarifa hii, tembelea tovuti ya Mradi wa Vitabu wa Global Voices na jihusishe!
1 maoni