Bahraini: Ali Abdulemam, mwanablogu na mchangiaji wa Global Voices akamatwa

Ali AbdulEmam


Ali Abdulemam, mwanablogu maarufu wa nchini Bahraini na mwandishi wa Kitengo cha Utetezi cha Global Voices, amekamatwa mapema leo na mamlaka ya nchi ya Bahraini kwa kile anachotuhumiwa nacho kwamba anasambaza “habari za uongo” kupitia mtandao wa BahrainOnline.org, ambao ni moja ya mitandao maarufu zaidi nchini humo inayopigania kuwepo kwa demokrasi zaidi, huku kukiwa na harakati mbaya zaidi ya zote za Serikali ya nchi hiyo za kuendeleza ubaguzi mbaya wa kiimani kwa miaka mingi sasa, pamoja na madai ya kuwepo kwa mtandao wa kigaidi unaowahusisha wanasiasa na wanaharakati wa haki za binadamu kadhaa. Mtandao huu wa BahrainOnline unachujwa sana na serikali ya Bahrain. Alituma barua-pepe mapema leo akieleza kwamba alipigiwa simu na maafisa wa usalama wa taifa wa Bahraini muda mfupi kabla hajakamatwa, na baada ya hapo walimkamata wakisingizia kwamba alikuwa akijaribu kutoroka.

Inasemekana kwamba serikali ya Bahraini ina rekodi ndefu ya utesaji wale wanaoonekana kuwa wakorofi, http://bit.ly/9kZyJQ na vipindi vinavyorushwa na Televisheni vinavyochochea chuki na ubaguzi wa kidaraja ili kuhalalisha harakati zake za kukomesha upinzani.

Ali aliwahi kukamatwa hapo kabla kwa ajili ya habari aliyowahi kuchapisha kwenye mtandao wake, na amekuwa mchangiaji wa makala katika Kitengo cha Utetezi cha Global Voices na vilevile katika kile cha Lingua ya Kiarabu ya Global Voices.

Habari mpya #1:

Kampeni ya kwenye mtandao inayotaka aachiwe huru ipo hai sasa.

Habari mpya #2:

BahrainOnline.org imezimwa.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.