Kuna uvumi ulioenezwa jana nchini Msumbiji kwa njia ya mdomo, ujumbe mfupi wa maneno wa simu na hata kupitia Twita kuhusu mgomo. Msukumo ukiwa: gharama za maisha zisizo za “haki” – kuongezeka kwa bei ya mkate, maji na umeme. Wasomaji watakumbuka kwamba ongezeko la nauli za vyombo vya usafiri wa umma lililofanywa mwezi Februari 2008 lilisababisha kuwepo kwa machafuko na maandamano. Kwa hiyo, jiji lilijikuta katika hali ya wasiwasi mkubwa.
Wakati vyombo vya habari vikuu nchini humo vilipoanza kuripoti kuhusu yanayoendelea, leo asubuhi wanablogu na wanatwita tayari wameanza kuripoti juu ya matukio mbalimbali. Eduardopp Castro wa Elefante News anaandika [pt]
Ouvi na Antena Nacional e li nO País (primeiro pública, segundo privado) que a polícia não “recebeu nenhum pedido de manifestação popular” para hoje aqui em Maputo.
Mas a cidade está visivelmente mais policiada. E já teve bloqueio em Benfica, Xiquelene e Chopal.
Tem pouco chapa (vans) circulando por Mahotas. Já recebi telefonema de gente que voltou pra casa depois de esperar por transporte desde cedo, sem sucesso.
A preocupação é que se reedite 2008: os chapas fizeram uma manifestação que convulsionou a cidade.
Na manchete dO País, o motivo da agitação: Água e luz com novos preços a partir de hoje em todo país”.
Lakini jiji linaonekana wazi kuwa linalindwa na polisi wengi zaidi. Kulikuwa na vizuizi vya barabarani katika maeneo ya Benfica, Xiquelene na Chopal.
Kuna daladala chache tu zinazojulikana kama chapa [mabasi ya usafiri ya umma] zinazotoa huduma katika eneo la Mahotas. Nilipigiwa simu na watu waliorejea nyumbani baada ya kusubiri muda mrefu sana usafiri pasipo mafanikio, yaani tangu mapema asubuhi.
Hofu ni kuwa huenda yale ya mwaka 2008 yakajirudia: wafanyakazi wa mabasi ya chapas waliingia kwenye mgomo uliolitupa jiji katika mkwamo mkubwa.
Kichwa cha habari kikuu kilicho ukurasa wa mbele wa gazeti la O País, kile kinachochochea kupanda kwa jazba: bei mpya ya maji na umeme nchi nzima kuanzia leo”.
Mwanasosholojia Carlos Serra, ambaye alikuwa chanzo muhimu cha habari mwaka 2008, aliandika [pt]
Com voz calma, um representante do Governo esforçou-se no programa “Café da manhã” da Rádio Moçambique (7:30/8:00) por mostrar que o governo tudo tem feito para evitar que o preço do pão (mais caro a partir do dia 6, estável desde 2008) fique mais oneroso… Ouvintes do programa enviaram mensagens queixando-se da carestia de vida e lamentando a subida do preço do pão, “alimento do pobre”, escreveu um deles. O representante apelou aos ouvintes para procurarem substituir o pão por outros produtos, por exemplo pela batata doce.
pelos relatos que me vão chegando de vários pontos da cidade (Avenida de Moçambique, por exemplo), penso que esta é uma situação que vai exigir muito bom senso e grande prudência na gestão.
Kupima mambo kwa kutumia ripoti zinazonifikia kutoka katika pande mbalimbali za jiji (kwa mfano Mtaa wa Msumbiji), nafikiri ili kumaliza hali hii itahitajika busara na hekima kubwa.
Mtumiaji wa Twita, BarataJorge, aliripoti
Linhas de telefonia móvel congestionadas, na cidade de Maputo.
Mwingine anayeitwa TeknikNineMilli alisema
#Greve em maputo. É o q dá abusar das pessoas. A parte má, é q há gente a pilhar, vandalizar e etc.
Mtumiaji mahiri wa twita, Katembe, tayari anatuma taarifa za kusikika kwa milio ya bunduki, mawe yakitupwa na uharibifu ukifanyika katika maeneo ya watu maskini jijini, kama vile hapa
Na EN4, carros e autocarros a ser atacados com pedras” / “isto está mal, nem dá pra pôr um pé fora de casa (Chamanculo)”
Mwanahabari wa kujitegemea, Nastasya Tay alituma ujumbe wa Twita
Vurugu katika maeneo ya vitongoji. Risasi za mpira zinapigwa. Watu wanachoma matairi yaliyotumika katikati ya barabara, na moshi unaonekana ukipaa katika anga la Maputo kutokana na moto huo.
Jukwaa la uandishi wa kiraia kupitia mfumo wa Ushahidi tayari limeanzishwa na Jornal A Verdade (@verdademz). Mpaka sasa, tayari kuna matukio zaidi ya 50 na katika mengine kuna taarifa za vifo , wakiwemo watoto wawili waliopigwa risasi huko katika Barabara ya Lusaka.
Kupitia A Verdade [Ukweli, pt] kuna tamko limetolewa na Serikali ya Msumbiji, ikiwataka raia kuacha vurugu na kutulia, hasa kwa kuwa usiku unaingia.