Habari kuhusu Bahrain

  4 Oktoba 2009

Kutoka Bahrain, Redbelt, anatabiri mwisho wa kublogu.. kama tunavyojua.

Nchi za Kiarabu: Homa ya Mafua ya Nguruwe Yaendelea

  24 Julai 2009

Homa ya mafua ya nguruwe au H1N1 bado inatawala vichwa vya habari vya magazeti katika nchi za Kiarabu kwani wagonjwa wapya wanaendelea kugunduliwa na mamlaka za afya na kutangazwa katika vyombo vya habari kila siku. Huu ni muhtasari wa yale wanayoongea wanablogu huko Bahrain, Jordan, Misri na Syria.

Bahrain: Mabloga Waungana Kupinga Uamuzi wa Kufungwa Kwa Tovuti

  2 Februari 2009

Wanablogu wa Bahrain wameujia juu uamuzi wa Waziri wa Habari wa nchi hiyo wa kuzuia upatikanaji wa tovuti mbalimbali, kadhalika kuzuia matumizi ya tovuti vivuli [proxy sites] zinazoruhusu watumiaji kuperuzi tovuti nyingine zilizozuiwa na zana za kuchuja habari. Ayesha Saldanha anaangalia maoni kutoka Bahrain.

Palestina: Mawasiliano na Gaza

  8 Januari 2009

Katika mazingira ya kawaida bila kiwango kikubwa cha wanaojua kusoma, usambaaji wa intaneti husimama kati ya asilimia 13 mpka asilimia 15 (Gaza na Ukingo wa Magharibi kwa pamoja). Kutokana na mashambulizi yanayoendelea huko huko Gaza, uwezo wa kutumia intaneti umepungua sana. Japokuwa kuna idadi ndogo ya wanablogu wanaoandika moja kwa moja kutokea Gaza, wakazi wengine wengi wanatumia ujumbe wa maandishi wa simu za mkononi pamoja na simu nje ya nchi katika matumaini kwamba ushahidi wao utapata sehemu ya kuelezwa.

Bahrain: Raha na Karaha za Kusoma Ng'ambo

  26 Oktoba 2008

Ingawa Bahrain ina idadi kadhaa ya vyuo vikuu, vya umma na binafsi, raia wengi wa nchi hiyo hupata fursa ya kwenda ng'ambo kwa masomo ya shahada ya kwanza na hata zile za juu, mara nyingi kwa kutegemea ufadhili. Moja ya matatizo ya kwanza wanayokumbana nayo huko ughaibuni ni kwamba watu wachache tu hufahamu ni wapi Bahrain ilipo. Katika makala hii tunafuatilia uzoefu wa wanablogu watatu ambao ndiyo kwanza wamekwenda ng'ambo kwa masomo: kule Japan, Uingereza na Marekani na mwanablogu wa nne ambaye anasoma India kwa kipindi fulani hivi sasa.