Nchi za Kiarabu: Homa ya Mafua ya Nguruwe Yaendelea

Homa ya mafua ya nguruwe au H1N1 bado inatawala vichwa vya habari vya magazeti katika nchi za Kiarabu kwani wagonjwa wapya wanaendelea kugunduliwa na mamlaka za afya na kutangazwa katika vyombo vya habari kila siku.

Huko Bahraini, Silly Bahraini Girl (ambaye ni mimi) amerudi nyumbani na kushangazwa na kile alichokiona katika kiwanja cha ndege cha nchini mwake:

Ukweli wa jinsi sehemu hii ilivyogeuka na kuwa ya kiwendawazimu unakupiga usoni sekunde ile unapotua kwenye kiwanja cha ndege cha kimataifa na kuona wafanyakazi wa ardhini wamevaa vitambaa vya kitabibu kufunika pua, kuanzia wahudumu mpaka maofisa wa uhamiaji.
“Mna tatizo gani?” Ninawauliza. “Kuna maambukizi Bahraini?” Niliendelea kuuliza […] hali ilionekana kuwa ngumu na kiwango cha wendawazimu wa mafua haya ya nguruwe kilikuwa juu kuliko niliyokutana nao kokote nilikosafiri tangu matatizo haya ya nguruwe yalipoikamata dunia. Kwanini hapakuwepo hata mtu mmoja aliyevaa matambara haya kwenye viwanja vya San Fransisco, Chicago, Toronto na Heathrow ambako nilisafiri
katika majuma machache yaliyopita?

Bado tukiwa Bahraini, Sohail Al Gosaibi ananusa njama kwenye hewa, anaona kwamba kukuza sana madhara ya mafua ya nguruwe kunayanufaisha mashirika ya habari, watangaza biashara na viwanda vya madawa. Mwanablogu wa Kisaudia anaandika:

Vyombo vya habari siku zote hukuza hali ya mambo, kumbuka kwamba hofu huuza. Na magazeti na idhaa za habari ni lazima viuze nafasi za matangazo na muda wa kurusha matangazo hewani ili kutengeneza fedha, na kwa kadiri habari inavyokuwa inatishia na kuogopesha ndivyo wanavyopata watazamaji na wasomaji wengi zaidi, ambavyo huongeza watangaza biashara, na faida zaidi.

Al Gosaibi ananukuu makala aliyoisoma na kuhitimisha:

Kwa mujibu wa makala, Serikali za Marekani na Uingereza zina hifadhi ya madawa ya Tamifluiflu yenye thamani ya mabilioni ya dola ambazo lazima wazitumie ndani ya miezi michache ijayo, vinginevyo yatapita muda wake. Inafurahisha, eeh?

Na akizungumzia nadharia, mwanablogu wa Jordan Reform Watch pia anacho cha kusema na kuandika:

Ahhh..mafua ya nguruwe pamoja na nadharia zote za njama zinazoambatana nayo… “mwanasayansi” wa Kijordani bingwa wa magonjwa anadai kuwa Maka na Madina ziko mbali na ugonjwa huo, kwa hiyo hakuna haja ya kuzungumzia uwezekano wa mlipuko ambao unaweza kutokea kutokana na mamilioni ya mahujaji kuwa karibu karibu wakati wa hija…

Uweni nguruwe…Nendeni kwenye Hija…na mtakuwa mbali na ugonjwa…

Mwanablogu wa Kimisri Zeinobia, anayeblogu kupitia blogu ya Egyptian Chronicles, kadhalika anaguswa na jinsi ugonjwa utakavyosambaa wakati wa Haji [Msimu wa Hija ya Waislamu Maka kila mwaka], ambapo mamilioni ya mahujaji kutoka sehemu mbalimbali duniani hukusanyika Maka ili kutimiza nguzo hiyo. Anaandika:

majadiliano kuhusu mustakabali wa Hija na Omra [hija ndogo] mwaka huu bado ni suala linaloendelea. Waziri wa Afya anataka kuifuta Omra wakati Waziri wa Utalii anapinga kufutwa huko, sihitaji kuzungumzia kuhiji.
Ni kweli majadiliano ni makali miongoni mwa mashehe wa dini wenyewe. Saudia Arabia inaelewa changamoto iliyonayo tayari na imeamua kushughulikia hali hiyo kwa kadiri inavyoweza katika Omra na hija, inashauri kuwa mahujaji wajawazito, wazee na watoto waepuke kuhiji mwaka huu, Ninauheshimu uamuzi huu.
Pia ninalo pendekezo zuri zaidi. Katika mnazingira kama haya
kwa nini tusiwaruhusu tu wale mahujaji wa kwanza wake kwa waume kuhudhuria Omra na Hija.

Kituo chetu cha mwisho ni Syria, ambapo mwanablogu Yaser Arwani [ar] anatuunganisha na habari inayosema kwamba mgonjwa wa kwanza wa mafua wa nguruwe kuripotiwa Syria ilitaarifiwa na daktari wa Ki-Syria, anayefanya kazi Australia na alikuwa akiitembelea nchi yake. Daktari huyu wa kike alisafiri kwenda Syria kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Dubai na ugonjwa haukuwa umegunduliwa mpaka siku chache baada ya kuwasili kwake.

1 maoni

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.