Habari kuhusu Matangazo

Kufuatilia Kongamano la Dunia la Demokrasia 2013

  29 Novemba 2013

Kongamano la Dunia la Demokrasia kwa sasa linafanyika mjini Strasbourg, Ufaransa kwa mara ya ppili tangu lianze. Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “kuunganisha Taasisi na Wananchi katika Kizazi hiki cha dijitali”. Fuatilia mada nne na warsha 21 za mkutano kupitia alama ashiria #CoE_WFD. 

Mkutano wa Global Kampala, Uganda

Sauti Chipukizi  25 Novemba 2013

Mkutano wa Global Voices umepangwa kufanyika Novemba 23 jijini Kampala, Uganda, kuwaleta pamoja wanachama wa jamii hii kushirikisha mawazo.

Mkutano wa Global Voices Cairo, Misri

Sauti Chipukizi  16 Novemba 2013

Mkutano mwingine wa Global Voices unapangwa kufanyika Novemba 16 jijini Cairo, Misri. Tafadhali shiriki na wanachama wetu wa Jumuiya ya GV kwa kusanyiko hili maalumu.

Kusherehekea Mwaka 2012 na Sauti za Dunia

Kadiri mwaka 2012 unavyofikia tamati, tungependa kutoa shukrani zetu kwa kazi nzuri, ubunifu pamoja na kuonesha kujali mambo mengi katika jumuia ya Sauti za Dunia. Mwaka 2012 umekuwa ni mwaka wa ukuaji wa kasi kabisa na wa mafanikio kwa Sauti za Dunia ( Global Voices). Yafuatayo ni baadhi tu ya mafanikio:

Global Voices Yashinda Tuzo Ya Highway Africa

Timu ya Global Voices inayoandika habari za Nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara imeshinda Tuzo ya Telekom Highway Africa katika kundi la “Blogu bora ya TEHAMA ya Kiafrika”. Mhariri wa Eneo hilo Ndesanjo Macha alikuwepo Afrika Kusini kuipokea tuzo hiyo (na kikombe cha ushindi!) tarehe 11 Sepetemba,...