Timu ya Global Voices inayoandika habari za Nchi za Afrika zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara imeshinda Tuzo ya Telekom Highway Africa katika kundi la “Blogu bora ya TEHAMA ya Kiafrika”. Mhariri wa Eneo hilo Ndesanjo Macha alikuwepo Afrika Kusini kuipokea tuzo hiyo (na kikombe cha ushindi!) tarehe 11 Sepetemba, 2012 kwa niaba ya timu nzima. Mwanablogu na mwandishi wa habari Dorothy Dandejo kutoka Kameruni alikuwa mshindani wa karibu aliyeibuka mshindi wa pili katika kundi hilo hilo.
1 maoni