Global Voices Yaanzisha Ushirikiano na Shirika la Kukutanisha Wakimbizi

Refugees United

Wakimbizi Wakutanishwa

Hivi sasa dunia imeunganishwa zaidi kuliko ilivyowahi kuwa kabla, lakini wakati maelfu ya wakimbizi wanazikimbia nchi zao zenye migogoro au majanga na hivyo kupoteza mawasiliano na ndugu na jamaa zao -ambao mara nyingi hupoteza mawasiliano hayo milele. Katika wakimbizi 43 duniani kote, wengi wao wanasemekana hawaweza tena kuonana na familia zao tena kwa sababu tu ya kukosa namna ya kuwasiliana nao.

Refugees United[Wakimbizi Wakutanishwa] ni shirika ambalo hutumia mtandao wa intaneti na simu za kiganjani kusaidia familia zilizopoteana. Watumiaji wa mfumo wao huweka taarifa zao binafsi wanazoona ni salama kuzitangaza hadharani ambazo bado ziwafanye wabaki kuwa na faragha ya kutokufahamika. Watu wengi tayari wameshakutana na familia na marafiki zao kupitia mfumo huu wa Shirika la Wakimbizi Wakutana, lakini kuendelea kwa mafanikio hayo kutategemea ni jinsi gani wakimbizi watajua kuwa kuna kitu kama hicho.

Watafikiwaje?

Tangu mwaka uliopita, watafsiri wa Global Voices wamekuwa wakifanya kazi na shirika hilo la kukutanisha wakimbizi kwa kutafsiri vitendea kazi vyao, kutumia mitandao ya kijamii na ujumbe mfupi wa meneno (SMS) kwenda katika lugha za Kiswahili, Kifaransa, Kisomali, Kiamhari, Kiarabu cha Sudani na Kiarabu asilia. Tumeshirikiana nao kuwapa ushauri mahsusi kwa maeneo yanayolengwa kuhusu namna ya kutunga ujumbe unaoeleweka na unaokubalika kiutamaduni.

Shirika la Refugees United linasema linalenga kufikia watu milioni 1 ifikapo mwaka 2015 na Global Voices inajisikia fahari kutoa ushirikiano wa karibu.

“Ushirikiano na Global Voices ni ushahidi wa namna tunavyoweza kuzifikia familia nyingi zaidi kwa kushirikiana na mtandao wao imara wa watafsiri na wanablogu,” anasema Ida Jeng wa shirika hilo la Refugees United.

Nguvu ya kuungana kwa mara nyingine

Kwenye blogu ya Refugees United kuna masimulizi yasiyohesabika kuhusu miradi ya kuwafikia watu na namna watu waliopoteana walifanikiwa kukutana kwa mara nyingine.

Video hii inaelezaea simulizi la mwanamke aitwaye Estelle aliyekutana na dada yake baada ya kutengana naye kwa miaka 16.

Na video hii inawaonyesha kaka wawili wa ki-Kongo waliotengana kwa miaka 15 na hatimaye kukutana kwa mara ya kwanza kwenye zana ya mtandaoni ya Google Hangout on Air baada ya kufahamishana mahali walipo kupitia mtandao wa shirika la Refugees United.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.