Simulia Hadithi Yako Kupitia Programu ya StoryMaker na Ushinde €1,000

StoryMaker ni programu mpya iliyoundwa kuwasaidia watu kuunda na kubadilishana hadithi bora za habari kwa usalama na salama iwezekanavyo kupitia simu zao za mkononi. Programu hiyo tumizi hukuwezesha kuchanganya kwa usalama na kuhariri programu na elimu ya uandishi wa habari ya mpango ya kuboresha hadithi ya mkononi. Programu hiyo iko tayari kwa matumizi na inapatikana kwa kila mtu. Ili kuhamasisha watu wengi tuwezavyo kuanza kutumia StoryMaker, sisi tunaandaa mashindano. Shiriki kwa kutoa hadithi kupitia StoryMaker au kutupatia mapendekezo ya kuboresha.

Hadithi Bora

Tumia StoryMaker kuelezea hadithi yako na kushindania €1,000. Kila hadithi zinaingizwa kwenye www.storymaker.cc na moja kwa moja unashiriki katika shindano kwa ajili ya tuzo. Sisi twatafuta hadithi bora ambayo ingalikuwa haijasimuliwa bila hadithi ya mkononi.

Mapendekezo Bora ya Uboreshaji

StoryMaker imezinduliwa muda mfupi uliopita, lakini hiyo haimaanishi kwamba hakuna nafasi ya kuboresha. Kinyume chake, tunahitaji watumiaji wetu kuendelea kuboresha Programu hiyo. Tafadhali tutumie maoni yako, mawazo ya ubunifu, makosa uliyoyapata katika toleo la sasa na vinginevyo Kutusaidia kuifanya StoryMaker kuwa mafanikio ya kweli. Kuna tuzo la €1,000 kwa ajili ya wazo bora. Tuma barua pepe katika msaada [katika] storymaker.cc.

Unaweza kushiriki hadi Desemba 31, 2013.

Ushirikiano

StoryMaker imekuzwa na Free Press Unlimited, The Guardian Project na Small World News. Sasa inapatikana kwa Kiingereza na Kiarabu. Kila mtu anaweza kuanzisha tafsiri mpya, kuwezesha watu wengi zaidi duniani kote kutumia StoryMaker.

Soma kuhusu ushiriki wa Sauti za Dunia katika mradi wa StoryMaker

Imechapishwa kutoka Free Press Unlimited.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.