Mkutano wa Global Voices Cairo, Misri

gv-meetup-logo-gvmeetup-400Tunayo furaha kutangaza kwamba Mkutano wa pili wa Global Voices utafanyika Cairo, Misri kuanzia Novemba 16 kwa ajili ya warsha itakayokuwa inaanza saa 5 asubuhi mpaka saa 9 alasiri.

Kwa kawaida, Global Voices imekuwa na jumuiya imara ya waandishi wanaojitolea, watafsiri, na wahariri wanaoishi katika mji mkuu wa Cairo. Wanachama hawa wa jumuiya yetu wanahusika na miradi na harakati nyingi ya uandishi wa kiraia, teknolojia, na uandishi wa habari pia, na wamekuwa raslimali muhimu kwa wengijne wanaotaka kuwa wachapakazi katika eneo hili.

Kwa nyongeza, mwaka 2000, Mradi wa Rising Voices uliendesha shindano la kupata ufadhili wa miradi midogo midogo hususani kwa miradi ya kuwafikia waandishi wa kiraia kutoka Misri. Kwa minajili hiyo, tulifadhili na kuunga mkono miradi mitatu: Nazra, Wanawake wa Minya Siku kwa Siku, na Simulizi za Blogu ya Mokattam.

Mkutano huo utawaleta pamoja wanachama wengi wa jumuiya hii ili kuwawezesha kushirikishana uzoefu na kusaidia kuwezesha mitandao ya kirafiki miongoni mwao wenye maono yanayofanana. Ikiwa imeandaliwa na wanachama wetu wawili Mohamed El Gohary (@ircpresident) na Tarek Amr (@gr33ndata), pamoja na wanachama wengine wa GV, mkusanyiko huo utajikita kwenye:

  • Kutoa mtazamo wa jumla wa kazi ambazo tunazifanya kwenye Global Voices, ikiwa ni pamoja na Rising Voices, Advox, and Lingua
  • Kushirikishana mbinu ambazo jumuiya kubwa zaidi inaweza kuhusishwa na miradi ya Global Voices.
  • Kuunganisha shughuli kwa namna ambayo washiriki wanaweza kushirikishana taarifa kuhusu miradi yao wenyewe ya mtandaoni au hata maoni kwa ajili ya miradi
  • Kukuza matumizi ya mitandao ya kijamii katika kazi zao kwa kutumia uzoefu wa washiriki wengine

Kama ungependa kushiriki, tafadhali jaza fumu ya ushiriki, na timu yetu itakujibu kwa habari zaidi za kina, ikiwa ni pamoja na maelekezo kamili ya namna ya kufika mkutanoni. Tukio hili liko wazi kwa watu wote, lakini washiriki lazima waombe kuhudhuria kabla ya mkutano.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na: rising [at] globalvoicesonline.org

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.