Pitia tathmini zetu za kikanda za Sauti za Dunia (Global Voices) kwa mwaka 2012
Kadiri mwaka 2012 unavyofikia tamati, tungependa kutoa shukrani zetu kwa kazi nzuri, ubunifu pamoja na kuonesha kujali mambo mengi katika jumuia ya Sauti za Dunia. Mwaka 2012 umekuwa ni mwaka wa ukuaji wa kasi kabisa na mwaka wa mafanikio kwa Mtandao wa Sauti za Dunia. Yafuatayo ni baadhi tu ya mafanikio:
Jumuia yetu imekaribia kuwa mara mbili zaidi kwani Mtandao wa Sauti za dunia kwa sasa una takribani waandishi 700 na watafsiri 600 wa kujitolea na pia kuna zaidi ya watu 700 wanaotoa michango yao kwa kila mwezi.
Walioomba kupata ufadhili wa Sauti Zinazochipukia (Rising Voices) kwa misaada midogo ya kifedha kwa mwaka 2012 walifikia 1200, takribani ongezeko la karibu asilimia 50 ya kiwango cha mwaka 2011. Ongezeko hili ni utambulisho wa matokeo ya sauti za raia na vyombo vya habari vinavyofanya kazi kila mahali, hata sehemu zile mabazo zinakabiliwa na upungufu wa vifaa pamoja na changamoto mbalimbali za kijamii kiasi cha kushindwa kushiriki katika mitandao ya intaneti.
Tumefanikiwa kuweka kumbukumbu nzuri ya kutembelewa na watu 157,000 kwa siku moja.
Kongamano la Sauti za Dunia linalofanyika kila baada ya miaka miwili lililofanyika mwaka huu jijini Nairobi nchini Kenya, lilikuwa ni tukio lililokuwa na muitikio mkubwa na morali ya hali ya juu kiasi cha kushindwa kufananishwa na tukio jingine na lililotusaidia kuweka mikakati ijayo ya mtandao wa Sauti za Dunia.
Timu ya Utetezi wa Sauti za Dunia (Advocacy) imepiga hatua kubwa, kwa maudhui mapya, wanachama wengi wapya, na kuwa na dira ya dhati ya utendaji na mipango ya mwaka 2013. Timu hii Utetezi wa Sauti za Dunia linaingia mwaka 2013 likiwa na Mkurugenzi mpya ambaye ni ndugu Hisham Almiraat, anayeendeleza msingi imara ulioanzishwa na Sami Ben Gharbia.
Kuongezwa kwa lugha za Amharic na Kibulgaria mwaka 2012 kumesababisha idadi ya lugha katika Sauti za dunia kufikia lugha 35 zinazotafsiriwa katika mtandao huu. Kwa kuongeza, kadiri vyazo vyetu vya habari vinavyotumia lugha zaidi ya moja vinavyozidi kuongezeka, makumi mawili ya makala kila mwezi huwa zinaandikwa moja kwa moja kwa lugha nyingine mbalimbali zaidi ya Kiingereza.
Wakati idadi inaweza kuakisi uhalisia wa matokeo ya Sauti za Dunia, kwa dhati kabisa, tunapenda kusherehekea na kuwashukuru wote wanaojitolea na ambao kwa pamoja wanaifanya Sauti za Dunia kuwa na morali ya hali ya juu na kama jumuia ya kuaminika. Tunatamani tungekuwa na uwezo wa kuweka picha za kila mmoja, lakini, tupo wengi kweli kweli!
Heri ya Mwaka Mpya!
Georgia Popplewell na Ivan Sigal