j nambiza tungaraza · Juni, 2009

makala mpya zaidi zilizoandikwa na j nambiza tungaraza kutoka Juni, 2009

Honduras: Zelaya Akamatwa na Kuondolewa Madarakani

  29 Juni 2009

Nchini Honduras siku ilianza na habari zinazosema kwamba Rais Mel Zelaya amekamatwa akiwa nyumbani kwake na wanajeshi wenye silaha mnamo siku ya kupigwa kura tata ya maoni. Siku chache kabla, Zelaya alimuondoa madarakani mkuu wa majeshi. Maoni yanatofautiana kutokea yale yanayosema kwamba hali iliyopo ni sawa na mapinduzi ya kijeshi mpaka yale yanayosema kuwa hii ilikuwa ndio njia pekee ya kukomesha jitihada za Zelaya za kutaka kugombea urais kwa awamu nyingine tena.

Iran: Video za Maandamano ya Upinzani Zazidi Kumiminika

Zaidi ya watu 100,000 waliandamana mjini Tehran Jumatatu iliyopita ili kumuunga mkono mgombea urais mwanamageuzi, Mir Hussein Mousavi pamoja na madai yake ya kuataka kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi ambayo yalimtangaza rais aliye madarakani Mahmoud Ahmadinejad kama mshindi katika uchaguzi wa tarehe 12 Juni. Damu ilimwagika mwishoni mwa maandamano hayo. Watu wapatao 7 walipoteza maisha yao.

Irani: Maandamano na Ukandamizaji

Mamia ya maelfu ya Wairani mjini Tehran na katika miji mingine kadhaa wameandamana kumuunga mkono mgombea urais Mir Husein Mousavi huku wakiipuuza amri ya serikali inayokataza maandamano. Japokuwa huduma za Twita, FaceBook pamoja na YouTube zimezuiliwa kwa kuzimwa nchini Iran, Wairani wengi wamekuwa wakitumia tovuti-vivuli ili kuvizunguka vichujio vilivyowekwa na wanaripoti habari kadiri zinavyotokea. Utawala wa Irani pia umezuia huduma za jumbe za maandishi kwa kutumia simu za mkononi (SMS), kadhalika utawala huo unachuja tovuti kadhaa zinazoakisi maoni ya wanamageuzi.

Uchaguzi Wa Irani Katika Picha

Uchaguzi wa rais nchini Irani utafanyika tarehe 12 Juni. Ni watu wanne tu kati ya watu zaidi ya 400 waliojiandikisha ambao wamepewa idhini rasmi na Baraza la Walezi kuwa wagombea katika uchaguzi. Macho makali ya wanablogu-wapiga picha yamenasa nyakati na taswira katika mitaa ya Irani ambako watu walikuwa wakiwapigia debe wagombea wanaowapenda.