j nambiza tungaraza · Septemba, 2010

makala mpya zaidi zilizoandikwa na j nambiza tungaraza kutoka Septemba, 2010

Jamaika: Banton Ajitayarisha Kwenda Mahakamani

  19 Septemba 2010

YardFlex.com anaifuatilia kesi ya umiliki wa madawa ya kulevya inayomkabili Buju Banton na ambayo itaendeshwa siku ya Jumatatu huko Marekani. Kutokana na taarifa zinazosema kwamba washtakiwa wenzake wawili wameamua kuwa mashahidi wa serikali (upande wa mashtaka) blogu hiyo inasema: “Siku mbili zinazofuata zitakuwa ni za muhimu sana kwani Buju na...

Karibeani: Kwa Heri, Arrow

  19 Septemba 2010

Wanablogu wa Karibeani wanaomboleza kifo cha mmoja wa waasisi wa muziki wa soca katika kanda hiyo - Alphonsus Cassell, ambaye anayejulikana zaidi kama “arrow” – na ambaye kibao chake kikali, Hot, Hot, Hot kinapewa sifa ya kuutambulisha mtindo wa soca kwa kadamnasi duniani kote. Taarifa za habari zinathibitisha kuwa muimbaji huyo allikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa muda; rambirambi za wanablogu zimekuwa na mguso pia zinaelezea masikitiko binafsi...

Brazil: Uchaguzi Safi kwa Mtindo wa “Jifanyie Mwenyewe”

  11 Septemba 2010

Chini ya mwezi mmoja ujao kutakuwa na uchaguzi nchini Brazil na mradi wa Eleitor 2010 tayari umekwisha kuwa na nguvu za kubadili mchakato huo: ni mradi wa “vyanzo vya habari vya kiraia” ambao una lengo la kuratibu taarifa za raia zinazoripoti ukiukwaji wa mchakato wa uchaguzi nchini Brazil. Kwa kupitia jukwaa hilo, kuna simulisi kadhaa za kuburudisha ambazo zimeshaanza kujitokeza.