makala mpya zaidi zilizoandikwa na j nambiza tungaraza kutoka Februari, 2010
Chile: Tetemeko Kubwa la Ardhi lenye Ukubwa wa 8.8 Laikumba Chile
Saa 9:34 usiku kwa saa za Chile, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 8.8 liliukumba mwambao wa eneo la Maule nchini Chile. Tetemeko hilo liliutetemesha mji mkuu wa Santiago uliopo Kilomita 325 kutoka katika kiini cha tetemeko hilo. Uharibifu mkubwa umeripotiwa nchin nzima, na idadi ya waliofariki inazidi kwenda juu.
Mapinduzi Nchini Niger: Wanablogu Wapumua Pumzi ya Ahueni
Alhamisi Februari 18 mapinduzi ya kijeshi yalifanyika nchini Niger ambayo kwayo Rais Mamadou Tandja alikamatwa baada ya mapambano ya bunduki katika mji mkuu, Niamey. Miezi michache iliyopita Tandja alibadilisha katiba kinyume cha sheria ili ajiruhusu kuongoza kwa muhula wa tatu katika kile ambacho kilionekana kama dhuluma ya halaiki kwenye kura maoni. Wanablogu wanatoa mitazamo yao juu ya maendeleo haya mapya.
Vazi la Burka Lauelemea Utaratibu wa Tamaduni Mbalimbali Kuishi Pamoja
Tangu mapendekezo ya kupiga marufuku uvaaji wa burqa au hijab huko Ufaransa, suala hilo limekuwa likitokota katika ulimwengu wa bloghu wa Australia. Mtangazaji wa redio katika mtindo wa kushtua umma, ambaye pia ni askari polisi wa zamani, alishutumiwa hivi karibuni juu ya kupinga kuvaliwa kwa hilo vazi la burqa.
Ghana: Mapendekezo ya Kuvutia Kwenye Mapitio ya Katiba
Mwaka 2008, wakati wa Uchaguzi wa rais, wagombea waliwaahidi Waghana kuwa wangeitazama tena katiba ya nchi hiyo. Jambo lililoifanya ahadi hii kuonekana kama ni ya kweli lilikuwa ni nia ya wagombea – pamoja na Rais John Atta Mills – ya kuwashirikisha Waghana katika mchakato huo wa kuitathmini katiba. Inaonekana kuwa rais ametimiza ahadi hiyo, na sasa mapendekezo mapya yanachochea mijadala ya kuvutia.
India: Ugaidi Waikumba Pune
Mnamo majira ya saa 1:30 jioni (Februari 13, 2010) mlipuko wa bomuuliua watu 9 na kuwajeruhi wengine 57 katika mgahawa maarufu kwa watalii uliopo katika mji wa Magharibi wa Pune, India. Hisia ziko juu huku wanablogu na watumiaji wa twita wakitoa maoni.
Malaysia: Harakati za Kutovaa Nguo za Ndani Wakati Wa Siku ya Valentino
Wanafunzi kadhaa wa kike nchini Malaysia wanahamasisha "harakati za kutovaa nguo za ndani" katika siku ya Valentino. Kampeni hiyo imepata umaarufu mno kupitia ujumbe wa mtu kwa mtu na kwa kupitia intaneti. mamlaka za kidini hazijafurahishwa. Wanablogu wanatoa maoni.
Tangazo la Mkutano Mkuu wa Uanahabari wa Kiraia wa Global Voices 2010
Tunayo furaha kutangaza Mkutano Mkuu wa Uanahabari wa Kiraia wa Global Voices 2010! Mwaka huu mkutano wetu utafanyika katika mji mchangamfu wa Santiago, Chile tarehe 6-7, 2010.Kati ya vivutio vya mkutano huo kitakuwa ni kutangazwa kwa washindi wa Tuzo Ya Kuvunja Mipaka, tuzo mpya iliyoundwa na Google pamoja na Global Voices.
Haiti: Pesa Zinazotumwa na Ndugu na Jamaa Zasaidia Kabla ya Misaada Rasmi
Huku simu zikiwa zinaanza kufanya kazi tena nchini Haiti, pesa zinazotumwa na ndugu walio nje ya nchi “kwa waya” zinaanza kuwasili tena, na kusaidia ujenzi hata kule ambako mashirika ya kimataifa bado hayajafika. Pesa zinazotumwa na wanafamilia wanaoishi nje ya nchi, kwa uchache, zilikuwa kama asilimia thelathini ya Mapato ya Taifa ya Haiti kabla ya tetemeko la ardhi la Januari 12.