Colombia: maoni ya Awali Kuhusu Kifo cha Kiongozi wa FARC ‘Mono Jojoy’

Mapema siku ya Alhamisi tarehe 23 Septemba watu wa Colombia waliamka na taarifa ya habari hii: Siku iliyopita, ndege 30 na helikopta 27 za jeshi la Anga la Colombia zilivamia kambi ambamo Víctor Julio Suárez, ambaye anajulikana zaidi kama Jorge Briceño or Mono Jojoy, mmoja wa viongozi wa juu wa Majeshi ya Ukombozi wa Colombia (FARC), alikuwa amejificha pamoja na dazeni za wapiganaji gorila karibu na La Macarena, Meta. Suarez, mwenye umri wa miaka 57, aliuwawa katika kile kilichoitwa “Operesheni Sodoma”, kama ambavyo Rais Juan Manuel Santos alivyothibisha [es] kutokea mjini New york, ambako alikuwa akihudhuria mkutano wa Baraza la umoja wa mataifa. Askari watano wa majeshi ya Usalama walijeruhiwa na mbwa wa kike wa polisi aliuwawa [es].

Viongozi wengine wa juu wa wapiganaji hao gorila inawezekana kuwa walikamatwa ndani ya kambi hiyo yenye ukubwa wa mita za mraba 30 – ambayo inataarifiwa kuwa [es] ilikuwa na [es] mahandaki ya kuishi chini ya ardhi – na majeshi ya ulinzi ya Colombia (ambayo yalijumuisha zaidi wanajeshi wa jeshi la Colombia pamoja na Jeshi la Polisi la Taifa ambalo lilitua baada ya mapigano kumalizika) yanawafanyia utambulizi wakati makala hii ikiwa inaandikwa. Mnamo majira ya mchana siku ya Alhamisi vyanzo visivyo rasmi vilidai kuwa kiongozi wa FARC Henry Castellanos, Romaña, naye pia aliuwawa [es] katika operesheni hiyo.

Mono Jojoy, ambaye alitoswa na mdukizi, alikuwa akichukuliwa kama kiongozi wa upande wenye siasa kali katika jeshi la FARC na alikuwa kamanda wa Kanda wa Mashariki. Aliaminika kama “mmoja wa wapiganaji gorila mwenye uchu wa damu” [es],kulikuwa na hati 62 za kuamrisha kukamatwa kwake, aliwahi kuhukumiwa mara 5, na Marekani ilikwishaomba kukamatwa na kusafirishwa kwa mtu huyo kwenda Marekani kujibu tuhuma zinazohusiana na usafirishaji madawa ya kulevya, na iliahidi kutoa zawadi kwa kukamatwa kwake.

Utata uliibuka pale ambapo El Tiempo, gazeti la kila siku lenye wasomaji wengi zaidi nchini humo (ambalo linamilikiwa kwa kiasi na familia ya Rais Juan Manuel Santos’ ), lilipotuma mfululizo wa twita kuhusu habari hii:

@eltiempocom

Vigilantes de parqueadero en Corferias: ‘Hay que pedir la tarde libre para celebrar la muerte de Jojoy’

Walinzi wa maegesho ya magari ya Corferias: ‘Inatubidi tuombe mapumziko ya mchana ili kusherehekea kifo cha Jojoy’

@eltiempocom

¿Cómo están celebrando en sus oficinas o donde se encuentren la muerte de Jojoy?

Unasherehekea vipi kifo cha Jojoy hapo kazini kwako au popote pale ulipo?

@eltiempocom

Para los ofendidos por la pregunta de celebración, disculpas. Mejor pregunta es: ¿Cómo reaccionan por la muerte de Jojoy?

Kwa wale mliochukizwa na swali kuhusu kusherehekea, tunaomba radhi. Njia bora ya kuuliza: Je mmekipokea vipi kifo cha Jojoy?

Watumiaji wa Twita walijibu mara moja jumbe hizo za twita. Miguel Olaya (@juglardelzipa) alisema:

por ahora no nos han dado el día libre en la universidad de los andes. @eltiempocom debería denunciarlos por no ser patriotas.

Mpaka hivi sasa bado hatujapewa siku ya mapumziko hapa katika Chuo kikuu cha Los Andes. @eltiempocom linapaswa kuwalaani kwa kutokuwa wazalendo.

Mtumiaji mwenye jila la @PAPerezA alilikosoa gazeti hilo::

Que ignorancia y amarillismo!! Salvajes!! […]

Ujinga na ushabiki ulioje!! Washenzi!!

Agnes Dantés (@Agnes_Dantes) alifanya mzaha:

Ayy esos de @eltiempocom son muy jocosos. Pero bueh… bien por ellos que no nos engañan con falsa imparcialidad y profesionalismo

ooooh jamaa wa @eltiempocom wanachekesha sana. Lakini… wamefanya vyema kwa kutokupotosha na [dhana ya] uwajibikaji usiofungamana na upande wowote na ustadi wa kazi wa uongo

Kwa kejeli, Clo Calao(@cloquis) aliandika:

Hay unos desplazados al frente de mi casa pidiendo limosna, les voy a preguntar a ellos como celebran la muerte de #jojoy #eltiempostyle

Kuna watu waliopoteza makazi wanaomba pesa mbele ya nyumba yangu, Nitawauliza ni kwa jinsi gani wanasherehekea kifo cha #Jojoy #eltiempostyle

Adriana (@Adridice) aliandika maoni kuhusu ombi la msamaha lililotumwa na El Tiempo:

las disculpas del @eltiempocom dejan mucho que desear “a los que se sientan ofendidos” que amarillismo, están peor que el espacio

ombi la msamaha la @eltiempocom halina mshiko, “wale waliochukizwa”, ushabiki na udaku mtupu, hawa ni wabaya zaidi ya El Espacio [gazeti la udaku linalochapishwa kila siku]

Wengine walilitania jina la operesheni, ambalo kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi Rodrigo Rivera lilichaguliwa [es] kwa sababu “kiini cha uovu kilikuwa pale. Na tulihitaji msaada kutoka mbinguni.” Orlando (@DanielitoBang) alisema:

Alejandro Ordóñez abrirá investigación contra Rodrigo Rivera y la cúpula militar por usar el aberrante nombre de Sodoma en esta operación.

[Mkuu wa Jeshi la Polisi] Alejandro Ordóñez atamchunguza Rodrigo Rivera pamoja na uongozi mzima wa jeshi kwa kutumia jina potofu la ‘Sodoma’ kwenye operesheni hii.

Ramírez Jaramillo (@egolaxista):

La película de la Operación Sodoma será clasificada R, porque su nombre es sugestivo

Filamu kuhusu Operesheni Sodoma itakuwa na kiwango cha R (filamu yenye maudhui ya watu wazima), kwani jina lenyewe linaashiria hivyo

Kwa mzaha tu, Miguel Olaya (@juglardelzipa) aliandika:

en el ministerio de defensa organizan focus groups para decidir el nombre de las operaciones.

Pale Wizara ya Ulinzi vikundi mahsusi vya tafiti vinaandaliwa ili kuchagua majina ya operesheni

Alvaro Sáenz (@AlvarettoS):

:o que el mono jojoy murió de sodomía? #toomuchinformation

:o je Jojoy alifariki kutokana na ulawiti (u-sodoma)? #toomuchinformation

Maoni mengine katika twita yanashabihi masuala yaliyopo katika siasa za Colombia. Manuel Carreño (@Popcultura) alielekeza ujumbe wake kwa wale wanaoipinga serikali ya sasa na ile iliyopita:

Amigo antiuribista: alegrarte por esta noticia no te vuelve de derecha: solo demuestra que te alegras por la muerte de cafres como ese.

Rafiki anti-uribista: kuhisi furaha kutokana na taarifa hii hakukufanyi uwe mtu mwenye siasa za mrengo wa kulia: kunaonyesha tu kwamba unafurahia kifo cha mwanaharamu kama huyu.

Lakini Juan C. Rodríguez (@JCRodriguezMD) hadhani kwamba matokeo ya operesheni hii ni ishara ya kuwa serikali imefanikiwa:

El éxito de un gobierno no se mide por número de bajas, sino por el bienestar de su población. En eso si seguiremos muy mal.

Mafanikio ya serikali hayapimwi kwa idadi ya adui waliouwawa, bali kwa ustawi wa watu wake. Katika [suala] hilo, tutazidi kufanya vibaya.

Mtumiaji wa twita @Vulturno alisema:

Sin duda es el logro más grande de las FFMM, con todo y que les tocó matarlo de lejos y con sevicia

Hapana shaka hili ni fanikio kubwa zaidi ya yote ya Majeshi ya Wapiganaji, haidhuru kwamba ilibidi wamuuwe kutokea mbali na kwa unyama

Daniel Arango (@stultaviro) alielezea mafanikio ya operesheni hii yanamaanisha nini kwa watu wa Colombia:

Qué buena bofetada a los que andaban anunciando y celebrando el fracaso de la Seguridad Democrática.

Kofi zuri lilioje kwa wale waliokuwa wakitangaza na kusherehekea kushindwa kwa Ulinzi wa Kidemokrasia

Katika ujumbe wake wa twita, Alejandro Gaviria (@agaviriau) anahusisha [kifo hicho] na dhana ya haki:

No es la muerte lo que alegra a la mayoría de la gente: es la idea o la sensación de justicia.

Siyo kifo [chake] ambacho kinawafanya watu wengi wafurahi: ni ile dhana au hisia ya haki

Lakini Orlando (@DanielitoBang) anafikiri kuwa haki haikutekelezwa vilivyo:

Qué rabia que mueran tipejos como ese. Se siente cierta sensación de justicia, pero el miserable en realidad murió impune.

Nimekasirika kwamba watu washenzi kama huyu wanakufa. Wewe unahisi kutendeka kwa namna fulani ya haki, lakini mwanaharamu huyu alifariki kabla ya kuadhibiwa

“El Chiflamicas” (@elchiflamicas) aliandika:

Si no mataban al Mono Jojoy se les hubiera escapado por algún aeropuerto.

Alieth Acosta (@_InTheMood) alikosoa shinikizo [lililojitokeza] la kuonyesha uzalendo:

Si no pongo una bandera de Colombia en mi nick de bb soy terrorista entonces? Esas bobadas.

Ikiwa sitabandika bendera ya Colombia kwenye [simu yangu ya kiganjani ya Blackberry] basi ni haki iibiwe kwa kuwa mimi ni gaidi? Upuuzi gani huo.

“La Morenita” (@lapetitebrune) alisema:

El día en que celebremos la vida, en vez de la muerte, ese día sí habrá esperanza para nosotros.

Siku ambayo tutasherehekea uhai, badala ya kifo, siku hiyo ndiyo patakuwepo na matumaini kwetu.

Makala nyingine zinazohusiana na hii:

Picha ndogo kutoka Wikimedia Commons: “Kazi hii ipo kwenye himaya ya umma nchini Marekani kwa sababu hii ni kazi mojawapo ya Serikali ya Marekani chini ya masharti ya sheria ya 17, Aya ya 1, Kifungu cha 105 cha Sheria ya Marekani. Angalia Haki Miliki.”

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.