That African Girl ni blogu yenye mfululizo wa makala zilizoandikwa na Waafrika duniani kote kuhusu maisha yao ya utotoni. Ni blogu juu ya kukulia katika familia ya kiAfrika na kujifunza kuishi katika dunia (au tamaduni) mbili. Wanablogu wanaoelezea kumbukumbu hizo wamewahi kuishi kote, Barani afrika na katika nchi za Magharibi.
Blogu hiyo ilianzishwa na Makafui Fiavi pamoja na Adey Teshome. Makafui alizaliwa nchini Togo na alikulia nchini Marekani na Adei ni kijana mwenye asili ya Ethiopia-na-Marekani.
Huu ndio utangulizi wa Makafui:
Wakati wa miaka ya uanafunzi chuoni, watu wengi hujipa muda wa kuzielewa nafsi zao zaidi pamoja na nafasi yao ulimwenguni. Watu wengi hufanya hivyo kwa kujaribu namna tofauti za kujitambua, au kwa kuvinjari makundi tofauti ya kijamii na kiitikadi. Kwangu, miaka ile 4 ilinipa fursa ya kuvinjari utambuzi wa nafsi zangu tofauti na hamu kubwa ya kutaka kujifunza jinsi ya kuishi kati ya tamaduni 2. Kuzaliwa na kukulia nchini Togo na kuendelea kukua nchini Marekani kumenipa hamu ya kuchunguza na kuelewa tamaduni mbalimbali, kusikiliza simulizi na kujifunza kuhusu mambo yanayowakutanisha watu. Msichana Yule wa kiAfrika (TAG) ni matokeo ya dhana, mazungumzo na hamu ya kuendelea kujifunza na kushirikiana masomo yaliyoyojitokeza. Hapa ndio sehemu ninayoelezea kuhusu vitu, watu, mahali, simulizi, ndoto pamoja nay ale yanayonivutia moyoni na ambayo yananipa ari.
Adey Teshome anaichukulia blogu kama “sehemu ya watu wa tamaduni mchanganyiko, wenye kuvutiwa na masuala anuai, (sehemu) ya watoto wa kipekee kama sisi kupaza mawazo yetu”:
Mwanzoni nilipokubali kuandika katika blogu hii, nilihamasishwa sana na wazo la Mak – sehemu ya watu wa tamaduni mchanganyiko, wenye kuvutiwa na masuala anuai, (sehemu) ya watoto wa kipekee kama sisi kupaza mawazo yetu. Na kama ninavyopenda kusema, hii ndiyo sababu sisi ni maraki. Ana jicho zuri la kujieleza na mitizamo mizuri ya kueleza. Na nililipenda wazo la kuwa sehemu ya mchakato huo. Na hivyo ndivyo ninavyojaribu kuwa katika blogu hii – kijana mwenye asili ya kiEthiopia na Kimarekani, mhitimu (aam, anayetarajia) kuhitimu mafunzo ya chuo, anmbaye anajaribu kuijua nafasi yake katika na kupata msingi katika maisha, ambaye anaweza kuchangia senti mbili za mawazo kila inapowezekana.
Liz A. ni mchangiaji kutoka Uganda/Kenya ambaye anaishi nchini Marekani.Na hizi ndizo kumbukumbu zake za utotoni:
1)Kuchapwa kama adhabu. Mara zote niliona kama jambo la kuvutuia pale marafiki zangu wa Kizungu au Kiasia walipokuwa wanaongelea adhabu ya kuketi kwenye kona, au walipoamriwa kwenda chambani kama adhabu. Kwetu, tulikuwa tunapigwa. Mama kwa kawaida alikuwa akiokota fimbo nyembamba zilivyoanguka kutoka kwenye miti iliyokuwa ndani ya boma letu na baba alikuwa akiokota zile kubwa, wakati mwingine tulitumwa kwenda kuzileta sisi wenyewe, na tulikuwa tunachapwa kwenye sehemu ya viazi nyuma ya ugoko.
Nchini Marekani, inaonekana kuwa jambo kama hilo linaweza kusababisha taasisi za huduma za jamii kuitwa ili kutathmini hali, au watoto hapa huweza kuhisi namna fulani ya kuwachukia wazazi wao kutokana na adhabu kama hizo. Lakini mimi
1 maoni