j nambiza tungaraza · Februari, 2009

makala mpya zaidi zilizoandikwa na j nambiza tungaraza kutoka Februari, 2009

Dunia Nzima: Lugha 2,500 Zinapotea

  28 Februari 2009

Ramani shirikishi ya lugha zinazopotea, inayoonyesha lugha 2,500 kati ya 6,000 ambazo ziko hatarini, imezinduliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO). Shirika hilo la kimataifa linawaomba watumiaji wachangie kwa kutuma maoni kwenye mradi huo ambao unawatia mashaka wanablogu wengi wenye nia ya kuhifadhi tamaduni.

Sudani: Maombolezo ya Mwandishi Maarufu wa Riwaya na Mahakama ya Kimataifa

Baada ya kimya kirefu, wanablogu wa Kisudani, wamerejea kwenye ulimwengu wa blogu kuongea, na kubadilishana mawazo kuhusu matukio ya hivi karibuni. Mawazo hayo yanayojumuishwa katika muhtasari huu ni pamoja na yale ya wanablogu tuliowazoea. Baada ya malalamiko kuhusu hali mbaya ya usalama wa afya kwenye Uwanja wa Ndege wa Khartoum, Msudani mwenye matumaini anaomboleza kifo cha mwandishi wa riwaya mashuhuri, Al- Tayeb Saleh.

India: Filamu ya Slumdog Millionaire Yanyakua Tuzo za Oscar

  27 Februari 2009

Filamu ya Danny Boyle, Slumdog Millionaire, iliyotokana na kitabu chenye maudhui ya India imefanya vyema katika sherehe za 81 za tuzo ya Academy. Wahusika wake kutoka Uingereza na India walitia kapuni zawadi 8 ikiwemo ile ya Picha Bora. Kwa hakika ilikuwa ni siku ya India, kwa kuwa filamu nyingine fupi...

Clinton Azuru Indonesia

  26 Februari 2009

Pamoja na kukutana na viongozi wa Indonesia, Katibu wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton alipata muda wa kutembelea makazi ya watu masikini mjini Jakarta. Kadhalika alitokea kwenye kipindi cha televisheni cha vijana. Ni nini maoni ya wanablogu?

Misri: Wanablogu Wafuatilia Milipuko ya Mabomu Mjini Kairo

  26 Februari 2009

Mtalii wa Kifaransa ameuwawa na watu wapatao 20 wamejeruhiwa wakati bomu lilipolipuka nje ya msikiti wa Al Hussein uliopo katika eneo la utalii la Khan Al Khalili mjini Kairo. Na wakati dunia ilipokuwa inaanza kufahamu ni kipi kilichokuwa kinatokea, wanablogu wa Misri waliingia kazini haraka, wakipashana habari za yanayotukia, taarifa, uchambuzi na hofu zao.

Martinique: Uhuru na “Ubeberu” wa Kifaransa

  26 Februari 2009

Wakati harakati za wafanyakazi zinaendelea huko Martinique na Guadeloupe, wanablogu wa Martinique wanapima uhuru wa Idara za Ng'ambo utamaanisha nini. Le blog de [moi] anaona dhana ya kuwa Martinique haiwezi kujitegemea ni dhana inayotusi na ya kibeberu. Wasomaji wake wanadhani kuwa ukweli wa kisiwa chochote kidogo ni kuwa kila siku kitakuwa katika kivuli cha wengine.

Guadeloupe: Hali Tete Yazua Ghasia

  26 Februari 2009

Baada ya wiki za maandamano ya amani katika Idara za Ng'ambo za Ufaransa za Guadeloupe na Martinique, mambo yaligeuka na kuwa ghasia siku ya jumatatu, polisi na waandamanaji walipambana katika jiji kubwa la Guadeloupe, Pointe-a-Pitre. Wafanyakazi wanapinga ukosefu wa ajira unaoongezeka pamoja na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu, ambazo nyingi zake huagizwa kutoka Ufaransa.

Indonesia: Talaka na Ndoa za Mitala

  22 Februari 2009

Najihisi nina hatia ninapoandika kuhusu talaka na ndoa za mitala wakati wa siku ya wapendanao ya Valentino. Lakini mada hizi zisizotamkika ni ukweli wa mapenzi na mahusiano. Katika Indonesia, wanawake wengi wanawataliki waume zao kwa sababu ya mitala.

Paraguai: Wahamiaji Wasimulia Visa Vyao

  22 Februari 2009

Ni jambo la kawaida katika Marekani ya Latini kwa wahamiaji kuondoka na kwenda kwenye malisho ya kijani zaidi kwenye nchi jirani au nchi za mbali. Hakuna tofauti kwa Waparaguai, ambao huwaacha nyuma marafiki zao na familia ili kufuata fursa nyingine. Simulizi kadhaa za namna hiyo zinasimuliwa kwenye blogu inayoitwa Paraguayos (sisi ni Waparaguai), ambayo inawaalika wahamiaji walioko duniani kote kuwasilisha simulizi zinazohusu uzoefu wao.