Clinton Azuru Indonesia

Katibu wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton aliwasili nchini Indonesia Jumatano iliyopita. Alitilia mkazo “jukumu la Indonesia katika kudhibiti matatizo ya dunia, yanayojumuisha ugaidi, uchumi wa kujihami, mabadiliko ya hali ya hewa(kuongezeka kwa joto) na matatizo ya kiuchumi.” Indonesia ndio taifa kubwa la Kiislamu duniani na nchi ya tatu kwa ukubwa kati ya zile zinazoongozwa kidemokrasia.

Pamoja na kukutana na viongozi wa Indonesia, Clinton alipata muda wa kutembelea makazi ya watu masikini mjini Jakarta. Kadhalika alitokea kwenye kipindi cha televisheni cha vijana.

Bloga Everything Indonesia anaamini kuwa ziara ya Clinton nchini Indonesia inafungua zama mpya ya sera ya nje ya Marekani:

Ziara ya katibu wa Mambo ya Nje wa Marekani Clinton nchini Indonesia inafungua zama mpya za sera ya nje ya Marekani. Sera iliyopungua dharau, inayojumuisha zaidi kama inavyoitwa nguvu-zenye-akili.

Bloga Mbak Rita amegundua kwamba Clinton anaonekana kijana sana leo:

“kwa kweli nafikiri anaonekana kijana na mrembo, pengine inatokana na tabasamu lake alilotoa wakati wa ziara yake hapa… Watu wengine katika kipindi cha maongezi cha televisheni nilichokitaja kabla walisema kwamba watu wa Jakarta walijawa jazba za bure kuhusu ziara yake. Nafarijika kuwa nilikosea.”

Devi Girsang alishangazwa na hali ya barabarani siku aliyowasili Clinton:

Kama mkazi wa Jakarta niliyozoea kukwama kwenye foleni za magari, huwa nafadhaika kama barabara zikiwa tulivu na zenye watu pungufu. Ni mambo mawili yaliyoingia akilini mwangu; kuna vitisho vya mabomu au ghasia. Unakumbuka machafuko ya Jakarta ya mwaka 1998 au shambulio la Hoteli ya Marriot la mwaka 2003? Umeshahamu namaanisha nini

Majira ya saa 8 za mchana leo, iliondokea kuwa ni kuwasili kwa Katibu wa Mambo ya Nje wa Marekani mjini Jakarta ndio kulikosimamisha magari. Bahati yangu nilikuwa bado nina mawe kwenye kamera yangu ya kidijitali nikaweza kupiga picha kadhaa.

Katika safu ya maoni, Therry, anajiuliza kama Marekani ilimtuma Clinton wa uongo:

Niliangalia hotuba aliyoitoa Clinton kwenye televisheni na sina hakika kama ni mimi tu, lakini yule mwanamke hafanani na Hillary.

Naanza kufikiri kuwa serikali ya Marekani ilimtumia Clinton wa uongo, kwa sababu yule mwanamke anaonekana mzee sana na jimama kuwa Clinton wa kweli.


Siyo kila mmoja aliyeshangilia ziara ya Hillary Clinton nchini Indonesia. Picha kutoka kwa Jakarta Today.

Andreas Harsono alitaka Clinton aongelee masuala ya uhuru wa kidini, usawa katika sheria na mageuzi ya kijeshi wakati wa ziara yake:

“(Clinton) awe muangalifu na asiseme kuwa Waislamu wa Indonesia wana “siasa za wastani” kama wanavyosema wanadiplomasia wageni. Kwa wanachama wa makundi ya kidini yanayokandamizwa nchini Indonesia, tamko hilo halina maana na ni kauli mbiu potofu.

“Mashaka ya ongezeko la kutokuvumiliana kidini sio suala pekee ambalo Clinton angeliongelea na Rais Susilo Bambang Yudhoyono. Uhuru wa kujieleza pia ni tatizo kubwa katika visiwa vidogo ambako makabila madogo yanaonyesha upinzani kwa dola ya Indonesia. Katika Indonesia, hata vitendo vya amani kama vile kupandisha bendera vinaweza kukupeleka jela kwa muda mrefu.

Clinton anaweza kushawishika kupamba masuala kama uhuru wa kidini, usawa katika sheria na mageuzi ya kijeshi ili kuboresha uhusiano wa Marekani na Indonesia. Na kama akifanya hivyo, atapoteza fursa ya kubadilisha maisha ya watu wengi nchini Indonesia ambao wanataka serikali ishinikizwe kutambua haki zao.

Kupitia huduma ya Twita yafuatayo ni maoni yanayohusu ziara ya Clinton:

waxinglyrical: kuna mtu ameuliza hillary Clinton ni nani?

mirageinblue: Nimemuona hillary clinton mapokezi. Safi sana

oplet: Klabu ya mashabiki wa Obama wanafanya maandamano kumopinga Hillary Clinton mjini Jakarta, wanasema hawampendi tangu wakati wa kugombea nafasi ya kugombea urais.


Picha kutoka ukurasa wa Flickr wa Idara ya Mambo ya Nje ya Marekani

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.