Habari kuhusu Iran

Iran:Raia wa Mtandaoni Wanane Wakamatwa

  2 Novemba 2013

Mamlaka ya Iran ilitangaza kuwa raia wa mtandaoni wanane ikiwa ni pamoja na mwanamke mmoja walikamatwa katika Rafsanjan, katika Mkoa wa Kerman, kwa madai ya “kutusi utakatifu wa Kiislamu na maadili”.

Iran: “Mauaji” ya Wapinzani wa Iran 52 Wasiokuwa na Silaha

  5 Septemba 2013

Vikosi vya usalama vya Iraq vilifanya “mauaji” ya wapinzani  wa Iran wapatao 52 ambao hata hivyo hawakuwa na silaha  asubuhi ya Jumapili ndani ya kambi yao kaskazini mwa Baghdad, mujahedeen-e-Khalq, wafungwa wa Iran walisema. Netizens in Balatarin, tovuti maarufu ya kusambaza habarii, iliweka picha kadhaa, filamu na posti kuhusiana na shambulio...

Iran: Waziri Mpya wa Kigeni Yupo Kwenye Mtandao wa Facebook

  19 Agosti 2013

Waziri mpya wa Uhusiano wa Kimataifa wa Iran Mohammad Javad Zarif ana ukurasa wa Facebook ambapo huutumia kujibu maswali. Anasema “Mimi na watoto wangu huuhuisha (kuweka habari mpya) ukurasa huu.” Ukurasa huo una zaidi ya wafuatialiaji 79,854 walioupenda (wakati wa kutafsiriwa kwa posti hii). Mtandao wa Facebook hudhibitiwa nchini  Iran lakini ndio...

Iran: Utani Kuhusu Mdahalo wa Urais

  6 Juni 2013

Raia wa mtandaoni kadhaa walitwiti kuhusu mjadala wa pili wa rais na waliwakejeli wagombea. Potkin Azarmehr alitwiti “Wagombea urais wanaweza kuombwa kucheza muziki.”

Irani: Je, Dola Inamwogopa Msichana wa Miaka 13?

  30 Aprili 2013

Kuwapiga watu marufuku kusafiri nje ya nchi yamekuwa mazoea ya serikali ya Irani  kwa makusudi ya kuwaghasi wanaharakati wa asasi za kisiasa na zile za kiraia kwa miaka mingi. Lakini, mahakama ya usalama iliwasha moto upya kwa kumpiga marufuku kusafiri nje ya nchi mume wa mwanasheria wa haki za binadamu aliyefungwa Nasrin Sotoudeh pamoja na binti yao mwenye umri wa miaka kumi na mitatu, Mehraveh Khandan. Nasrin Stoudeh amehukumiwa miaka kumi na moja gerezani.