Waziri mpya wa Uhusiano wa Kimataifa wa Iran Mohammad Javad Zarif ana ukurasa wa Facebook ambapo huutumia kujibu maswali. Anasema “Mimi na watoto wangu huuhuisha (kuweka habari mpya) ukurasa huu.” Ukurasa huo una zaidi ya wafuatialiaji 79,854 walioupenda (wakati wa kutafsiriwa kwa posti hii). Mtandao wa Facebook hudhibitiwa nchini Iran lakini ndio uliotumiwa na wagombea wote wa urais katika uchaguzi uliopita.