Habari kuhusu Iran kutoka Oktoba, 2010
Irani: Ziara ya Rais Ahamdinejad Nchini Lebanoni
Rais wa Irani, Mahmoud Ahmadinejad, amemaliza ziara yake ya siku mbili nchini lebanoni. Ilikuwa ni ziara yake rasmi ya kwanza tangu mwaka 2005 wakati alipochukua madaraka. Alikuwa na mazungumzo na maofisa wa Lebanoni na alizuru ngome za maswahiba wa Irani. Alipata mapokezi ya shujaa. Wanablogu kadhaa wa Irani walitoa maoni kuhusu ziara hiyo.
Urusi: Wanablogu wakutana na Balozi wa Irani, waepa kuhoji masuala nyeti
Mkutano kati ya wanablogu wanaoongoza nchini Urusi na Balozi wa Irani jijini Moscow, siku tatu tu baada ya mwanablogu Hossein Derakshan kuhukumiwa kifungo cha miaka 19.5 jela kwa kile kilichoelezwa kuwa ni "kufanya propaganda zinazoipinga serikali" ulizionyesha wazi juhudi zisizoeleweka za diplomasia ya mtandaoni ya Irani nchini Urusi. Vilevile ulionyesha jinsi maslahi binafsi ya kibiashara pamoja na mtizamo taharuki uliopita kiasi wa baadhi ya wanablogu maarufu wa Urusi.