Habari kuhusu Mazingira
Jinsi Raia wa Mynmar Wanavyokabiliana na Kupanda kwa Joto Kunakotokana na El Niño
El Niño tayari imeshasababisha ukame katika maeneo mengi ya Myanmar. Fuatilia kujua namna wakazi wanavyokabiliana na joto kali.
Namna Hali ya Hewa ya El Niño Inavyoathiri Maeneo ya Nyanda za Juu Nchini Myanmar
"Ziwa lililopo karibu na kijiji chetu lilikauka miezi miwili iliyopita. Mwaka uliopita, tuliweza kuchota maji katika ziwa hili hadi ilipofika mwezi Machi."
Yaliyojiri Wiki Hii Hapa Global Voices: Watetezi
Wiki hii, tunakupeleka Cambodia, Syria, Tajikistan, Gambia na Colombia.
Soga la “Twita” Laibua Hali ya Ukame Mbaya Kuwahi Kutokea Nchini Lesotho
"tatizo linaendelea kuwa kubwa, kwa hivyo inatubidi kukabiliana nalo kwa kutafuta ufumbuzi wa muda mrefu, sio kugawa cakula pekee."
Mwanaharakati wa Haki za Binadamu na Kiongozi wa Jamii za Wazawa Berta Cáceres Auawa nchini Honduras
Baada ya miaka kadhaa ya uanaharakati wa masuala ya mazingira na kuzitetea jamii za wazawa, mtetezi nguli wa haki za binadamu Berta Caceres ameuawa nchini Honduras hii leo.
Michoro Yaonesha Harakati za Raia wa Ufilipino Wakipambana na Ukandamizaji
Nchi ya Ufilipino ina idadi ya raia wazawa wanaokadiriwa kufikia milioni 14. Wengi wa raia hawa wanaoishi maeneo ya vijijini wapo katika hatari kubwa ya kuathiriwa na uharibifu unaotokana na shughuli za uchimbaji madini, harakati za utafutaji maendeleo pamoja na matumizi ya nguvu za kijeshi.
Wanaharakati Waomba Ulinzi kwa Makabila Yanayopinga Uchimbaji Madini Nchini Ufilipino
"Wao ndio waasisi wa tamaduni zetu za kipekee za sanaa. Mauji dhidi yao ni mauji ya utu wa watu wetu."
Wenyeji wa Visiwa vya Pasifiki Waizuia Meli za Makaa ya Mawe Kupinga Mabadiliko ya TabiaNchi
Kwa kutumia ngalawa zilizotengenezwa kwa mkono, washujaa wa mabadiliko ya tabianchi, wakishirikiana na raia wa Australia, waliweza kuzuia meli 10 zilizokuwa zitumie bandari ya Makaa ya mawe ya Newcastle.
Huduma za Afya nchini Madagaska Zinaweza Kukabiliana na Mlipuko wa Ebola?
Nchi kumi na tano za Afrika ikiwemo Madagaska ziko kwenye hatari zaidi ya maambukizi ya Ebola kwa sababu zina mazingira yanayofanana na yale ya nchi zilizoathirika. Waziri Mkuu anasema Madagaska imejiandaa lakini wengine wana wasiwasi
Filamu Yaonesha Namna Kabila Dogo Linavyojaribu Kuwazuia Wakata Misitu Kuharibu Mazingira
Sunset Over Selungo ni filamu ya dakika 30 inayoonesha namna kabila la wenyeji la Penan linavyopigania kutunzwa kwa misitu ya asili kwenye kisiwa cha Borneo nchini Malaysia. Borneo ni kisiwa kikubwa zaidi barani Asia. Filamu hiyo imetengenezwa na mtayarishaji huru wa filamu wa Kiingereza, Ross Harrison