Matangazo ya yaliyojiri wiki hii hapa Global Voices yanaangazia baadhi ya habari kubwa zilizojitokeza kwenye habari zetu za Global Voices.
Wiki hii tunakupeleka Cambodia, Syria, Tajikistan, Gambia na Colombia, ambako tunaongea kuhusu watetezi wanaolenda jamii zao na ukataji wa miti, upuuzaji wa mambo au udhaifu wa unaooneshwa na serikali na mabomu ya kikatili. Tunaongea na mhariri wetu wa Marekani ya Kusini Laura Vidal kuhusu kwa nini wakazi wa Medellín nchini Colombia wamebadili jina la jiji lao.
Shukrani nyingi kwa waandishi, watafsiri na wahariri wetu waliosaidia kufanikisha matangazo haya. Kipindi hiki kimechangiwa na habari zilizoandikwa na Mong Palatino, Echo of Truth, Amira Al Hussaini, Lara AlMalakeh, Demba Kandeh na Cati Restrepo. Tunasindikizwa pia na muziki wenye haki miliki ya Creative Commons kutoka maktaba ya Free Music, ikiwa ni pamoja na Jahzaar; Dramatic theme wa the PK Jazz Collective; All The Best Fakers wa Nick Jaina;You Know Who You Are wa Alan Singley; and Breathe in the Static wa Kirk Pearson and BIT.
Wasikilizaji wanaweza kusikiliza muziki wa Lean Street by Ketsa, uliotumiwa kwa ruhusa ya msanii mwenyewe.
Tarajiria kusikia sauti zetu baada ya wiki mbili.
Picha kwenye nembo ya Soundcloud ni ya mtumiaji wa mtandao wa Instagram danielup_, imechapishwa na maneno, “Mdoli mpya. Si kichekesho: Muhimu sana. Hasira.#Medehollín”.
Podcast: Play in new window | Download