Hii ni Makala kutoka The Irrawaddy, tovuti huru ya habari nchini Mynmar, na inachapishwa tena na Global Voices kama sehemu ya makubaliano ya kushirikiana maudhui.
Madhara ya mfumo wa tabia nchi wa El Niño hadi sasa umeshaonekana kwenye nchi kadhaa za Asia ya Pasifiki. Kadiri hali ya El Niño inavyozidi kushamiri hususani katika mzungunguko wa miezi 12 hadi 18, maeneno mengi ya Mynamar yameshazidiwa na joto la juu na ukame.
Kipindi cha ukame mara nyingi huwa kinaanza mwezi Machi, lakini hadi sasa, joto limekuwa la kiwango cha juu sana. Watabiri wa hali ya hewa wametabiri kuwa ukame katika maeneo mengi ya Myanmar utaongezeka hata kufikia mara tatu zaidi kwa miezi ijayo. Huko Yangon, eneo muhimu nchini Myanmar, joto limeshapanda hadi kufikia nyuzi joto 35 kwa siku za hivi karibuni, hali inayowalazimu watu kutafuta sehemu za ubaridi popote pale inapowezekana.
Huko Dala, mji unaokatisha mto kutoka Yangon, ukame upo wa hali ya juu sana. Wapiga picha wa Irrawaddy, Hein Htet na Pyay Kyaw hivi karibuni walielezea kwa picha namna wakazi wa Rangoon na Dala walivyokabiliana na hali mbaya ya hewa iliyoikumba Myanmar.