· Oktoba, 2009

Habari kuhusu Mazingira kutoka Oktoba, 2009

Trinidad & Tobago: Kampeni ya 350

  26 Oktoba 2009

“Trinidad na Tobago ni kisiwa tajiri na nchi inayoendelea tajiri kwa mafuta na gesi asilia. Lakini pia tunashuhudia madhara mabaya ya maendeleo ya haraka kwenye nyanja za viwanda katika visiwa vyetu. Hii ni fursa ya sauti za wanawake kusikika”: Attillah Springer anajihusisha na kampeni ya hali ya hewa 350.

Ghana: Siku ya Kublogu mwaka 2009

Kwenye siku ya Kublogu Kwa Vitendo Duniani, Waghana waliwahoji viongozi wa dunia, walichachafya karatasi za Benki ya Dunia, walitambulisha tovuti mpya na walijiuliza ni kwa nini kulikuwa na majadiliano machache sana yanayohusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa nchini – na pia walitambua kwamba kuna mambo fulani nchi kama Ghana zinayafanya vyema.