Habari kuhusu Asia
Unamjua Muuaji Mkuu Nchini Georgia? Ni Barabara Zake
Mnamo Machi 22 huko Tbilisi, mama mmoja pamoja na mtoto wake wa kike waliokuwa wamesimama kando ya barabara waligongwa na gari. Msichana huyo wa miaka 11 alipoteza maisha papo hapo.
Kilicho cha Zamani ni Kipya: Unasikiliza? Matangazo ya Sauti
Katika matangazo haya ya sauti, tunakupeleka hadi Jamaica, Indonesia, Syria, Macedonia na Ethiopia kwa simulizi za kumbukumbu, ufufuaji na uzima mpya
Wapenzi wa Nyumba, Hivi Ndivyo Nyumba za Umma Zinavyoonekana Japani
Blogu nzuri mahususi kwa kumbukumbu za miradi ya zamani ya nyumba zilizokuwa makazi ya vizazi kadhaa vya wa-Japani tangu kumalizika kwa vita vya dunia
Hali ya Uchafuzi wa Mazingira Kathmandu Imefanya Miungu Kuvikwa Barakoa
Kiwango cha Uchafuzi jijini Kathmandu kimezidi kiwango cha chini kinachokubaliwa huku wakazi wa jiji hili wakikabiliana na hali kwa kujizuia kwa mabarakoa, kama ilivyo kwa sanamu za watu maarufu zilizomo jiji humo.
Maisha Ndani ya Kituo cha Kulelea Watu Wenye Ukoma Nchini Myanmar
Pyay Kyaw anawatembelea wagonjwa kwenye kituo cha kulelea watu wenye ukoma cha Mt. Yosefu Cotto Legnos, kinachowatunza watu wengi, mmoja wao Maya, ambaye aliwahi kulazimishwa kwenda kuishi kwenye makaburini kwa sababu ya unyanyapaa.
Kikundi cha ki-Islam Chadai Kuondolewa kwa Sanamu Mbele ya Mahakama Kuu Nchini Bangladesh
Mamlaka zimepewa chini ya juma moja kufanyia kazi madai ambayo wakuu wa serikali na watumiaji wa wanayaona kama hayana maana
China Kufungia Kutolewa kwa Huduma ya Mitandao Binafsi ya Intaneti
Serikali ya China imefungia baadhi ya huduma za VPN China tangu 2015, lakini sera mpya inafanya kutumia VPN na huduma za intaneti zisizosajiliwa kuwa kosa
Jeshi la Nchini Thailand Lawaruhusu Watoto Kucheza na Bunduki halisi, Vifaru na Helikopta za Kijeshi
"Tunawawezesha watoto walifahamu vyema jeshi pamoja na zana zinazotumiwa. Kwa uzoefu wanaoupata, wanajifunza kulipenda jeshi na hata kuwa wanajeshi hapo baadae."
Siku ya Maombolezo Mjini Kyrgyzstan Kufuatia Ajali ya Ndege ya Mizigo, Iliyoua Watu Zaidi ya 30
Waliopoteza maisha wengi wao ni wenyeji wa Kyrgyz kutoka kwenye kijiji cha jirani, na habari zaidi zinaendelea kupatikana.
Upendo Unashinda Chuki: Kipindi cha Yaliyojiri Wiki Hii Hapa Global Voices
Wiki hii, tunaanzia Marekani ambapo Omar Mohammed anaelezea msemo wake, "Marekani niliyozoea kukupenda" na kisha kukupeleka Cuba, Syria, na Taiwani.