Nchini Japan, kuna blogu zinazojikita kwenye kuweka kumbukumbu za sehemu za ndani za gari moshi, vifuniko vya mashimo ya maji machafu na hata keki. Kwa hiyo hakuna ajabu kuwa kuna ukurasa wa Tumblr na blogu iliyojikita kwenye danchi (団地), ambazo ni nyumba za kale zilizokuwa makazi ya wa-Japani wengi tangu mwisho wa vita vya pili vya dunia.
Blogu hii ya Danchi inaangazia taswira zisizozoeleka za namna watu wengi wa Japani walivyoishi siku za nyuma, hata leo.
Neno danchi linaweza kuwa na tafsiri hasi kwa Wajapani, likifanana na maneno kama “miradi” au “nyumba za umma” kwa Kiswahili. Kwa Kijapani cha zamani, neno hilo linaweza kuwa na maana ya koei jutaku (公営住宅), au nyumba za serikali kwa Kijapani.
Concrete lovers, this blog explores the housing estates of Japan. Also known as ‘danchi’https://t.co/YvZgQsTwCL pic.twitter.com/vybt7p6bki
— Present & Correct (@presentcorrect) March 22, 2017
Wapenda nyumba, blogu hii inaangazia nyumba za nchini Japani. Pia ikifahamika kama ‘danchi’
Kama inavyojadiliwa kwenye jukwaa la tovuti ya Kimarekani MetaFilter, Kutembea kwenye Danchi !! ni blogu inayoandikwa kwa Kijapani ikilenga kuweka picha za nyumba nchini kote Japani. Blogu hiyo huwekwa habari mpya mara kwa mara, na inakuwa na picha za nyumba kutoka kila eneo nchini Japani, ikiwemo Kyoto, katikati ya jiji la Tokyo, Osaka na maeneo mengine ya Japani. Posti zinakuwa na taarifa kuhusu anuani kamili ya makazi, na lini yalijengwa:
Nyumba za Tamachi Ekimae (1966)
Shiba, Kata ya Minato, Tokyo
Picha zimepigwa 2016
Nyumba za serikali Osaka Kadoma (1967)
Kadoma, Wilaya ya Osaka
Picha zimepigwa 2017
Picha hizi zinakuwa zinaonesha hali kama ilivyokuwa nyakati za zamani wanazokumbuka watu walioishi kwenye nyumba hizi, kama vile milango iliyotengenezwa kwa vyuma vizito vinavyofanana na vile vilivyo kwenye nyambizi:
Naha Municipal Tsubogawa-East Apartments (Built 1985-1992)
Tsubogawa, Naha (Majengo ya Okinawa)
Picha zimepigwa 2016
Picha zinaonesha jitihada zilizochukuliwa hivi karibuni kupendezesha maeneo ziliko nyumba hizo za kale za umma nchini Japani.
Nyumba za Shirika la Nyumba Osaka Kadoma (1967)
Kadoma, Wilaya ya Osaka
Picha zimepigwa 2017
Nyumba za Shirika la Nyumba Osaka Kadoma (1967)
Kadoma, Wilaya ya Osaka
Picha imepigwa 2017
Akiandika makala kwenye jarida la Japan Times, Philip Brasor anaonesha kielelzo muhimu kwa makazi ya umma nchini Japani , ikiwemo sera ya nyumba ya serikali tangu nyakati za Vita vya Kwanza vya Dunai, inayotumika kwa makali ya umma nchini Japani, na namna serikali ilivyowekeza kidogo kwenye makazi kwa siku za hivi karibuni, ikiwemo kuongezeka kwa kazi za hatari na kuporomoka kwa posho vinavyosababisha kuongezeka kwa pengo la kipato nchini Japan.