Upendo Unashinda Chuki: Kipindi cha Yaliyojiri Wiki Hii Hapa Global Voices

Wiki hii, tunaanzia Marekani ambapo Omar Mohammed anaelezea msemo wake, “Marekani nilizoea kukupenda” na kisha kukupeleka Cuba, Syria, na Taiwani, kwa habari za mapenzi na uhuru wa kujieleza kwenye nyakati za uadui na hata chuki.

Kipindi cha Yaliyojiri Wiki hii kinaangazia baadhi ya habari kubwa zilizojitokeza zaidi hapa Global Voices. Tunakuletea watu, maeneo mapya na matukio kutoka duniani kote ambayo hayapewi uzito wowote unaostahili.

Shukrani nyigi kwa Omar Mohammed, I-Fan Lin, Budour Hassan, Andrea Chong Bras na Sara Holmes na Firuzeh Shokooh Valle na waandishi wetu wote, watafsiri na wahariri waliotusaidia kufanikisha kipindi hiki.

Katika kipindi hiki, tunasindikizwa na muziki wenye haki miliki ya Creative Commons kutoka maktaba ya Free Music, ikiwa ni pamoja na Please Listen Carefully wa Jahzaar;I’m what you’d be without her wa Doctor Turtle; Solitude wa Jahzarr, Crying Earth wa Kai Engel; na I fell too much in love wa Nick Jaina.

Shukrani nyingi kwa mwandishi wetu wa Global Voices Andrea Arzaba kwa kutusaidia kuandaa muziki.

Picha iliyotumika kwenye makala haya imechukuliwa kwenye maandamano ya kumpinga Trump jijini New York mnamo Novemba 12, 2016. Picha ya B.C. Lorio (CC BY-NC-ND 2.0).

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.