Hali ya Uchafuzi wa Mazingira Kathmandu Imefanya Miungu Kuvikwa Barakoa

Kiongozi mwanamke wa Kitibeti akisali huku akiwa amejizuia uso kwa barakoa ili kujikinga na vumbi katika nyumba ya kitawa ya Tharlam, Boudha, Kathmandu, Nepal. Picha kutoka Flickr na Wonderlane. CC BY-NC 2.0

Mji mkuu wa Nepali, Kathmandu unashuhudia uchafuzi mbaya wa hewa kuwahi kutokea katika historia ya uwepo wake. Vumbi likiwa limetapakaa kila mahali, magonjwa ya njia ya hewa yakiwa yanazidi kushamiri, huku serikali ikiichukulia hali hii kama ya kawaida kabisa na bila kuchukua tahadhari, kundi moja la wanafunzi limeamua kukabiliana na hali hii kwa kuvalisha vibarakoi sanamu za watu mashuhuri zilizopo katika maeneo mbalimbali ya jiji.

Hatimaye! Sanamu yavikwa barakoi na vijana kama namna ya kuonesha kutokukubaliana na uchafuzi wa hewa huko Kathmandu, Nepali

Wakazi waliunga mkono mpango huu kwa kutwiti viungo habari vyenye muunganiko wa ‘Kathmandu’ na'vumbi'; na ‘barakoi'na ‘Kathmandu’. Hata miungu katika onesho lililoandaliwa na Baha na Bahi ya Nepali , nyumba kubwa ya kitawa ya Kibudha na inayofahamika sana, walivaa mabarakoa.

Picha za sanamu ya Wazari Mkuu wa zamani wa Nepali Juddha Shamsher akiwa amevaa barakoi zilisambazwa sana mtandaoni.

Siamini katika kuharibu mali ya serikali, lakini hili lina lengo la kuikumbusha serikali kuhusu duskmandu

Kiwango cha uchafuzi wa hewa jijini Kathmandu kimezidi kiwango kinachokubalika na Shirika la Afya Duniani. Ujenzi mpya unaoendelea kufuatia tetemeko la ardhi la mwaka 2015, miradi ya upanuzi wa barabara sambamba na mradi wa ujenzi wa bomba unaohusishwa na Mradi uliosubiriwa sana wa Melamchi wa Usambazaji Maji (MWSP) imeongeza kiwango cha uchafuzi unaotokana na mamia ya vinu vya matofali vilivyopo katika maeneo mbalimbali ya jiji pamoja na msongamano wa magari katika barabara za Kathmandu.

Kwa mujibu wa Mtandao wa Hewa Safi wa Nepali.mbo la bakuli la bonde la Kathmandu linazuia pia kusafiri kwa upepo na hivyo kusaidia kuvuta uchafu kwenye anga, hali inayopelekea hatari kubwa ya uchafuzi wa hewa wakati wa baridi.

Afisa wa Kitengo cha Utafiti wa Afya nchini Nepali alieleza kuwa anga la Kathmandu lina kiasi cha dutu za uchafu chini ya maikrometa 2.5 (PM2.5), zinazoweza kusababisha kansa.  Dutu zilizo na kipenyo kisichozidi maikrometa 10 , ambacho ni kidogo kuliko unene wa unywele wa binadamu, ni vidogo mno kiasi cha kuweza hata kuingia kwenye mapafu na kuweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya.

Kipimo cha Uchafuzi wa Bonde

Chapisho hili la Instagram linaonesha #Vumbimandu.

#Dustmandu ! #Ringroad section at #Gausala, filled with #dust ! #melamchi #kathmandu #Nepal

A post shared by KinG Ashoka (@ashokpillar) on

Upendra Shrestha alichapisha kikaragosi hiki:

Hali halisi ya Dustmandu

Wakati serikali ingalikuwa imeshachukua hatua ili kukabiliana na ongezeko hili la vumbi, kwa sasa inakabiliana kwa taratibu sana kuhusiana na janga la uchafuzi.

Hivi karibuni, serikali ilipiga marufuku magari yaliyodumu kwa miaka 20 katika mji mkuu na maeneo yanayolizunguka bonde. Kwa mujibu wa ripoti ya BBC,kamati ya Uhifadhi wa Mazingira ya Bunge pia  imeiamuru Mamlaka ya Maji kunyunyiza maji ili kupunguza uchafuzi unaotokana na vumbi; pia vinu 10 vya matofali vimeanza kutumia teknolojia mpya inayolenga kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kinachokadiriwa kufikia 60%.

Hata hivyo, kwa sasa wakazi wa Kathmandu hawana njia mbadala zaidi ya kuvaa barakoi za kufunika nyuso zao, kama ilivyo kwa sanamu za kihistoria zilizopo jijini Kathmandu.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.