Habari kuhusu Uchumi na Biashara kutoka Disemba, 2011
Madagaska: Wajadili Uhalali wa Uwekezaji wa Kigeni wa Moja kwa Moja
Wakati Madagaska ikijaribu kutafuta suluhisho la matatizo ya muda mrefu ya kiasa, Wanablogu wa ki-Malagasi wanajadili thamani ya Uwekezaji unaofanywa Moja kwa Moja na raia wa Kigeni. Wa-Malagarasi wanaamini kwamba Madagaska, kama nchi nyingine za Kiafrika inao utajiri mkubwa wa rasili mali lakini tatizo likiwa ardhi yenyewe kupokonywa kwa sababu ya utawala mbovu na biashara zisizoangalia maslahi ya wananchi.
Zambia: Rais Sata Aituhumu Benki Kuu Kuchapisha Noti Bandia
Rais Michael Sata ameweka wazi kwamba Benki Kuu ya Zambia kwa maelekezo ya kilichokuwa chama cha Upinzani nchini humo MMD, ilichapisha “noti bandia” ambazo inasemekana ziko kwenye mzunguko wa fedha. Hata hivyo, Chama cha MMD kwa kupitia Waziri wake wa zamani wa Fedha Situmbeko Musokotwane, kimekana tuhuma hizo kikisema Benki Kuu inayo uhuru wa kuchapisha noti mpya za ziada bila kuwasiliana na Waziri wa Fedha ama Rais kwa sababu ina mamlaka kamili ya kufanya hivyo.