Habari kuhusu Uchumi na Biashara kutoka Februari, 2013
Mgomo wa Nchi Nzima Wamshitua Rais wa Malawi
Rais wa Malawi Joyce Banda atupilia mbali shinikizo la kujiuzulu mara baada ya mamia ya maelfu ya wafanyakazi wa umma kuandamana kwa wiki mbili kuishinikiza serikali kuongeza mishahara, hali iliyopelekea kufungwa kwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Malawi na kusababisha hali ya taharuki mahospitalini na mashuleni.
Bulgaria: Gharama Kubwa za Nishati Zasababisha Maandamano
Ruslan Trad anataarifu kuwa, siku ya Jumapili tarehe 17 Februari, makumi ya maelfu ya watu katika mji mkuu wa Bulgaria, Sofia pamoja na majiji mengine waliendelea na maandamano kupinga bei kubwa za nishati ya umeme pamoja na gharama za kupasha joto.