· Februari, 2009

Habari kuhusu Uchumi na Biashara kutoka Februari, 2009

Guadeloupe: Hali Tete Yazua Ghasia

  26 Februari 2009

Baada ya wiki za maandamano ya amani katika Idara za Ng'ambo za Ufaransa za Guadeloupe na Martinique, mambo yaligeuka na kuwa ghasia siku ya jumatatu, polisi na waandamanaji walipambana katika jiji kubwa la Guadeloupe, Pointe-a-Pitre. Wafanyakazi wanapinga ukosefu wa ajira unaoongezeka pamoja na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu, ambazo nyingi zake huagizwa kutoka Ufaransa.