Habari kuhusu Uchumi na Biashara kutoka Oktoba, 2012
Zambia: Filamu yaYouTube Kuhusu Athari za Machimbo ya Madini
Filamu ya Uchunguzi yenye jina "Zambia: Shaba Nzuri, Shaba Mbaya" inayohusu machimbo ya shaba nchini Zambia na athari zake kwa jamii imewekwa kwenye mtandao wa YouTube na mpaka sasa imevuta watazamaji zaidi ya 6,000. Baada ya kuitazama filamu hiyo, mtumiaji mmoja wa mtandao wa YouTube aliandika, "Jililie eeh nchi yangu nzuriKwa nini tubaki masikini katikati ya utajiri huu wa madini yanayochimbwa kwa gharama ya afya za wenyeji?"
Côte d'Ivoire: Wafanyakazi wa Afya Wagoma baada Miezi Minne Bila Mshahara
S.B anatoa maoni juu ya kuanza kwa mgomo usio na ukomo unaoratibiwa na wafanyakazi wa taasisi za afya mjini Abidjan. Katika mtandao wa Connection Ivorienne, anabainisha [fr] kwamba: Kufuatia mabadiliko...