Habari kuhusu Uchumi na Biashara kutoka Machi, 2010
Serikali ya Japani: Kuhusu Kuanguka kwa Mfumo wa Ajira
Chombo kinachotumika kufanya tafakari nzito cha Baraza la Mawaziri la Japani, Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (内閣府 経済社会総合研究所)(ESRI) kimechapisha matokeo ya utafiti yaliyopima hadhi ya sasa ya ajira...
Jamhuri ya Dominika: Upinzani Dhidi ya Shughuli za Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Barrick
Kumekuwa na ongezeko la upinzani dhidi ya shughuli za Kampuni ya Uchimbaji Dhahabu ya Barrick kwenye Jamhuri ya Dominika kwa sababu ya vipengele vilivyo kwenye mkataba na manufaa ya dola hilo, vilevile kutokana na sababu mbalimbali za kimazingira.
Mali: Vitambaa Vyasuka Nguzo za Uchumi na Utamaduni
Kwa kupitia video, tunaona na kujifunza kuhusu umuhimu wa utamaduni na ongezeko la kiuchumi ambalo utengenezaji vitambaa huwapa baadhi ya watu na mashirika nchini Mali. Vikundi vya wanawake, wasanii na watalii wote wananufaika na utamaduni huu wa kutia rangi vitambaa na upakaji rangi kwa kutumia matope.
Mwaka Mmoja Baada ya Mapinduzi, Viongozi wa Madagaska Wakabiliwa na Vikwazo
Machi 17, 2009 nchini Madagaska, vikwazo vinavyowalenga viongozi wa sasa wa Madagaska vinaandaliwa kwa kushindwa kwao kuheshima makubaliano ya Maputo ambayo hapo awali yalifikiwa na pande zote zinazohusika. Matokeo ya vikwazo hivyo ni pamoja na kuzuiwa kwa mali zinazozalisha fedha na pengine kukamatwa kwa wanaohusika endapo watasafiri nje ya nchi.
Chile: Tetemeko la Ardhi Lafichua Ukosefu wa usawa Katika Jamii
Ukiukwaji sheria kulikojitokeza baada ya tetemeko la ardhi la Februari 27 nchini Chile kumezua mjadala wa kitaifa kuhusu kutokuwepo kwa usawa wa kijamii na kiuchumi nchini.