Habari kuhusu Uchumi na Biashara kutoka Aprili, 2013
Bangladesh: Jengo Laporomoka, Mamia Wauawa kwenye Vifusi
Janga jingine tena la kiwanda nchini Bangladesh, safari hii jengo la ghorofa tisa lilianguka na kuua zaidi ya watu 142 na watu wengine karibu elfu moja kujeruhiwa. Watu wengine wengi bado wamenaswa kwenye kifusi na harakati za kuwaokoa bado zinaendelea. tukio hili linatokana na uzembe wa baadhi ya watu kwani utawala wa kiwanda hiki uliwashinikiza watu kuendelea kufanya kazi katika jengo ambalo halikuwa salama.