Habari kuhusu Uchumi na Biashara kutoka Julai, 2013
Je, Ziara ya Obama Barani Afrika ni Neema au Hasara?
Rais wa Marekani Barack Obama amemaliza ziara yake ya siku sita katika nchi tatu za Kiafrika, Senegali, Afrika Kusini na Tanzania, mnamo Julai 2, 2013. Obama alitangaza mradi mpya, "Umeme Afrika", kukuza matumizi ya umeme mara dufu katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara. Maoni ya watu duniani kote juu ya umuhimu na matokeo ya ziara hiyo yamegawanyika mno.