Habari kuhusu Majanga kutoka Januari, 2010
Haiti: Kituo Cha Habari Chazinduliwa Kwa Ajili Ya Uanahabari wa Haiti
Réseau Citadelle anatangaza kuzinduliwa kwa Kituo Cha Habari, mradi unaotoka kwa Wanahabari Wasio Na Mipaka pamoja na Quebecor, wenye lengo la kuwezesha kazi za wanahabari wa ndani na wa nje...
Lebanoni: Watu 90 Wanahofiwa Kufariki Baada ya Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia Kuanguka Baharini
Rambirambi zilimiminika kwenye Twita baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia kuanguka kwenye (bahari ya) Mediterani dakika chache baaday ya kupaa ikitokea Beirut, Lebanoni. Watu wote 90 waliokuwemo wanahofiwa kuwa wamekufa baada ya ndege hiyo kushika moto katika kimbunga cha radi na kuangukia baharini.
Haiti: Ramani za Kwenye Mtandao Zaonyesha Uharibifu Pamoja na Jitihada za Kusambaza Misaada
Marc Herman anaziangalia kwa karibubaadhi ya ramani ambazo watoaji misaada wanazitumia ili kuwasilisha hali inayobadilika kila wakati katika maeneo ya tetemeko la ardhi nchini Haiti. Karibu ya juma moja baada ya janga kutokea - na matetemeko yaliyofuatia ambayo yalifanana na matetemeko mengine makuu – ramani na taswira za setilaiti zinajidhihirisha kuwa ni taarifa pekee ambazo zinaweza kutegemewa.
Marekani: Raia wa Haiti Wapatiwa Hadhi ya Hifadhi ya Muda
Hadhi ya Hifadhi ya Muda (inayojulikana kama TPS) ni hadhi maalumu inayotolewa na Marekani kwa raia wa kigeni wanaotoka katika nchi fulanifulani ambamo kunakuwa kumetokea aina fulani ya janga au pigo la karibuni, kama vile vita au tetemeko la ardhi. Jana, Utawala wa Rais Obama ulitoa hadhi hiyo kwa raia wa nchi ya Haiti itakayotumika kwa kipindi cha miezi kumi na nane ijayo. Jillian C. York anapitia jinsi suala hili lilivyopokelewa katika blogu mbalimbali.
Haiti: Uenezaji Habari na Taarifa
Sisi tulio nje ya Haiti tunaweza tu kujenga picha kichwani kuhusu hali halisi ya maisha ya kila siku yalivyo huko baada ya tetemeko baya la ardhi - lakini katikati ya juhudi za kuwatafuta wapendwa ndugu, juhudi za kuwahudumia waliojeruhiwa na jukumu zito na gumu la kuwafikishia msaada wa kiutu wale wanaouhitaji zaidi - wanablogu walio huko Port-au-Prince na maeneo ya jirani wanawasiliana na ulimwengu wa nje, ambao nao unahangaika kutaka kupata taarifa kutoka kwa wale waliokuwa katika eneo lenyewe kabisa la janga.
Haiti: Twita Kutoka Eneo La Tukio
Wakati habari za tetemeko la ardhi huko Haiti zikitoa mwangwi duniani kote, wakazi majasiri, wanahabari wan je, na wafanyakazi wa misaada wanaandika jumbe za twita kutokea katika eneo lililoathirika. Baadhi yao wanafanya kazi ya kukusanya misaada na fedha, wakati wengine wanajaribu tu kuionyesha dunia mambo yanavyooendelea nchini Haiti.
Haiti: Madhira ya Tetemeko la Ardhi
Mpaka sasa taarifa za majeruhi wanaotokana na tetemeko la ardhi lililoikumba Haiti zimejikita kwenye takwimu za kutisha, lakini ni majina machache tu ndiyo yameambatanishwa kwenye namba hizo. Katika makala hii tunapata simulizi za wale walionusurika kutoka kwenye janga hili la asili kama wanavyozirusha kwenye mtandao.
Baada Ya Tetemeko la Ardhi, Jumbe za Twita Kutoka kwa Walioshuhudia
Kutokana na janga la tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 ambalo limekikumba kisiwa cha Haiti jioni ya leo (Januari 12), “Haiti” ni mada kuu hivi sasa kwenye huduma ya Twita. Miongoni mwa lundo la jumbe zinazotumwa tena na tena za taarifa za habari kutoka za vyombo vya habari vikubwa na jumbe nyingine za twita zinazotuma sala au dua pamoja na salamu za heri kwa kisiwa hiki cha Karibea, pia kumekuwepo taarifa za mashahidi waliopo kwenye tukio kama vile mwanamuziki na mwendesha hoteli Richard Morse, ambaye anatwiti kwa jina la @RAMHaiti.
Haiti: Maoni ya Mwanzo Kuhusu Tetemeko la Ardhi Lenye Ukubwa wa 7.0
Posti ya kwanza ya blogu iliyoandikwa kwa lugha ya Kifaransa kuhusu tetemeko la ardhi huko Haiti imetokea nje ya nchi hiyo, ikitangaza habari mbaya za kuanguka kwa Kasri ya Rais,...