Wakati habari za tetemeko la ardhi huko Haiti zikitoa mwangwi duniani kote, wakazi majasiri, wanahabari wan je, na wafanyakazi wa misaada wanaandika jumbe za twita kutokea katika eneo lililoathirika. Baadhi yao wanafanya kazi ya kukusanya misaada na fedha, wakati wengine wanajaribu tu kuionyesha dunia mambo yanavyooendelea nchini Haiti. Kadhalika wengine wanaripoti juu ya matukio katika maeneo fulani fulani, huku wakiwa na matumaini ya kuwaondoa hofu ndugu na wapenzi walio nje ya nchi (mpaka hivi sasa, ni taarifa chache mno zilizokwishatolewa kwenye wavuti kuhusu waliofariki na waliojeruhiwa).
Mapema leo, watu wengi walioko kwenye eneo la tukio walikuwa wakiandika jumbe za twita juu ya vurugu na ukosefu wa mipango inayoeleweka kunakoendelea hivi sasa. @fredodupoux anasema:
@bhatiap aliandika kuhusu kukosekana kwa uwepo wa polisi
@PIH_org (Wabia katika Afya) ambao wako huko Boston wanajitahidi kuwatafuta madaktari, hasa madaktari wa mifupa, ili kuwapeleka Haiti.
Baadhi ya watumiaji wa Twita wanaripoti juu ya majengo, mitaa au taarifa nyingine za muhimu kwa wale wanaotafuta familia zao au wale wanaojaribu kusafiri ndani ya nchi hiyo. @yatalley anaandika kuwa barabara inayotoka mji mkuu, Port au Prince, kuelekea mji wa Jacmel haipitiki.
@RAMHaiti amebaini uharibifu nkubwa kwenye sehemu za kuabudu. Anaripoti kuhusu kanisa moja la mjini Port au Prince, anasema:
@fredodupoux aliweza kwenda kwenye wilaya ya Delmas nje kidogo ya mji wa Port au Prince, eneo ambalo lilipokea athari kwa kishindo. Aliandika:
Kadiri ambavyo jumbe za twita zinavyozidi kutiririka, kuna njia nyingi za kuweza kufuatilia. @georgiap ametengeneza orodha ya watumiaji wa Twita walioko sehemu ya tukio nchini Haiti. Ninayo orodha nyingine ambayo pia ina majina ya mashirika ya misaada na wanahabari walioko kwenye eneo la tukio. Pia endelea kuangalia Ukurasa Maalum wa Haiti kwenye GV.