· Januari, 2009

Habari kuhusu Majanga kutoka Januari, 2009

Malaysia: Mafunzo Yanayotokana na Mafuriko

  21 Januari 2009

Wiki iliyopita, mafuriko yaliyakumba maeneo mbalimbali katika jimbo la Sarawak nchini Malaysia. Wanablogu wanaandika yaliyotukia na mafunzo yaliyotokana na janga hilo la mafuriko. Mafuriko hayo ni mabaya zaidi kutokea katika miaka mingi nchini Malaysia.

Palestina: Shule ya Umoja wa Mataifa Yashambuliwa na Makombora ya Israeli, Zaidi ya 40 wafariki

Takriban majira ya saa 12 za jioni (GMT +2), Idhaa ya Kiingereza ya Al Jazeera iliripoti kuwa shule moja ya Umoja wa Mataifa ilipigwa wakati makombora mawili ya vifaru yalipolipuka nje ya shule hiyo. Shule hiyo, iliyopo Jabaliya, ilianza kutumiwa kama makazi ya raia wa Gaza waliozikimbia nyumba zao au waliopoteza makazi yao. Zaidi ya watu 40 wameuawa. Jillian York anawasilisha maoni ya mwanzo kabisa katika ulimwengu wa blogu na twita.