Habari kuhusu Majanga kutoka Aprili, 2013
Bangladesh: Jengo Laporomoka, Mamia Wauawa kwenye Vifusi
Janga jingine tena la kiwanda nchini Bangladesh, safari hii jengo la ghorofa tisa lilianguka na kuua zaidi ya watu 142 na watu wengine karibu elfu moja kujeruhiwa. Watu wengine wengi bado wamenaswa kwenye kifusi na harakati za kuwaokoa bado zinaendelea. tukio hili linatokana na uzembe wa baadhi ya watu kwani utawala wa kiwanda hiki uliwashinikiza watu kuendelea kufanya kazi katika jengo ambalo halikuwa salama.
Uganda: Kukumbuka milipuko ya mabomu ya 2010
Wananchi wa Uganda wameutumia mtandao wa Twita na Facebook kuwakumbuka wahanga 2010 wa milipuko yha mabomu iliyotokea kwenye klabu ya Rugby huko Kyaddondo na katika baa ya Kijiji cha Kiethiopia jijini Kampala Uganda.Mashambulizi hayo yalitokea wakati ambao wapenzi wa kandanda walikuwa wakitazama mpambano wa fainali kati ya Uhispania na Uholanzi uliofanyika nchini Afrika Kusini.
Iran: Wakati Matetemeko yanaua, “Televisheni Zinafundisha Sala”
Matetemeko makubwa mawili ya ardhi yalilitikisa eneo la kaskazini magharibi nchini Iran, Mashariki jimbo la Azarbaijan mnamo Jumamosi (Agosti 11, 2012), na kuua watu 250 na kujeruhi karibu 1800. Matetemeko ya ardhi kipimo cha 6.4 na 6.3 katika ukubwa, na kusababisha uharibifu mkubwa na mateso. Wa-Irani waliingia kwenye mtandao wa intaneti ili kuwaombolezea wahanga na kuomba watu kujitolea damu na msaada. Pia walionyesha hasira zao kwa televisheni ya kitaifa ya Iran, ambayo hutangaza vipindi vya dini, badala ya kutoa taarifa kwa watazamaji kuhusu matetemeko ya ardhi na jinsi ya kusaidia.
Tanzania: Ghorofa Laporomoka jijini Dar Es Salaam
Pernille anaweka picha mtandaoni zinazoonyesha ghorofa lililoporomoka jijini Dar Es Salaam, Tanzania siku ya Ijumaa, 29 Machi 20013: “Karibu kabisa na jengo hilo kuna uwanja wa kandanda unaotumiwa na watoto....